• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 7:02 PM
Wageni wawili wakaa kizuizini uchunguzi ukiendelea

Wageni wawili wakaa kizuizini uchunguzi ukiendelea

NA RICHARD MUNGUTI

WAGENI wawili ambao uraia wao bado kutambulikana wanazuiliwa na polisi kwa siku 10.

Washukiwa hao Mcben Otaigbe na Kelvin Itowe waliagizwa wazuiliwe na hakimu mwandamizi Peter Mutua.

Akiwasilisha ombi la kuwazuilia rumande Konstebo Aaron Muema alimweleza Mutua kwamba anachunguza kosa la wizi wa mabavu.

Inadaiwa kwamba Otaigbe na Itowe walimshambulia na kumwumiza mpiga picha za video anayedai aliibiwa mkufu wenye thamani ya Sh1 milioni.

Kisa hicho, hakimu alifahamishwa, kilitokea katika makazi ya Casamia Apartment yaliyoko barabara ya Ngong, Nairobi.

“Washukiwa hawana hati za kuwatambua uraia wao na kiini cha kuwako humu nchini,” Konstebo Muema alimweleza hakimu.

Afisa huyo aliongeza kueleza korti washukiwa hao hawana makazi rasmi na wanaweza kutoroka wakati wowote.

Pia alisema anafuata kupokea ripoti ya hospitali ya mlalamishi.

“Kutokana na mawasilisho ya Konst Muema washukiwa hawana makazi rasmi na uraia wao bado haujulikani.Ombi la kuzuiliwa kwa siku 10 liko na mashiko kisheria na nalikubalia,” Bw Mutua aliagiza.

  • Tags

You can share this post!

Mchuuzi kutoka Sudan Kusini ashtakiwa wizi wa simu ya...

Wahudumu wa teksi mjini Thika watoa malalamishi ya kupokea...

T L