• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Wajerumani walikosa kuongeza idadi 2020

Wajerumani walikosa kuongeza idadi 2020

Na Mashirika

IDADI ya watu nchini Ujerumani ilikosa kuongezeka mwaka jana sababu ya janga la corona, ripoti ya serikali iliyotolewa jana inaonyesha.

Ripoti hiyo ya ofisi ya takwimu inasema hakukuwa na ongezeko la watu kati ya Januari na Desemba 2020, ikilinganishwa na 2019.Awali, ilidhaniwa kuwa vikwazo vilivyowekwa na serikali kuwataka watu wakae nyumbani ili kudhibiti maambukizi, vingesababisha idadi ya watoto kuongezeka nchini humo.

Lakini matokeo yanaonekana kinyume.Ni mara ya kwanza kwa idadi ya watu Ujerumani kukosa kuongezeka katika mwongo mmoja uliopita.Kwa mujibu wa ofisi hiyo ya takwimu, watu milioni 83.2 walikuwa wakiishi nchini humo kufikia mwishoni mwa 2020 – idadi inayokaribiana na ya 2019.

Kadhalika, vifo vilikuwa juu kuliko watoto waliozaliwa. Ingawa hivyo, mwaka huu watoto wanaozaliwa waliongezeka maradufu mwezi Machi, baada ya serikali kuondoa vikwazo vya corona.Kuanzia mwaka 2011 hadi 2019, idadi ya watu iliongezeka kutoka milioni 80.3 hadi 83.2m.

Serikali ilisema kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa iliongezeka maradufu Machi mwaka huu, baada ya serikali kuondoa vikwazo vilivyowekwa kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.Kadhalika, ofisi hiyo ilisema kuwa idadi ya vifo ilikuwa juu kuliko watoto waliozaliwa.

  • Tags

You can share this post!

Brazil kumalizana na Colombia leo usiku

Hakuna kondomu Team Kenya itakapotua Tokyo kwa Olimpiki