• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:50 AM
Hakuna kondomu Team Kenya itakapotua Tokyo kwa Olimpiki

Hakuna kondomu Team Kenya itakapotua Tokyo kwa Olimpiki

Na GEOFFREY ANENE

KWA mara ya kwanza tangu 1988, hakuna kondomu zitapeanwa kwa wanamichezo watakaoshiriki Olimpiki, makala ya 2020 yatakapofanyika Julai 23 hadi Agosti 8.Vyombo vya habari nchini Japan vimeripoti hayo saa chache kabla ya wenyeji kutangaza kuwa ni mashabiki 10,000 pekee nchini humo watakubaliwa kufika uwanjani kutazama michezo hiyo.Kenya itatuma zaidi ya wanamichezo 80 kutoka fani za riadha, raga, voliboli, taekwondo, uogeleaji na ndondi katika michezo hiyo ya mataifa 204 itakayojumuisha pia timu ya wakimbikizi chini ya Mkenya Tegla Loroupe. Zaidi ya wanamichezo 18,000 wanatarajiwa katika kambi ya Olimpiki mjini Tokyo.Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) ilisambaza kondomu 350,000 za wanaume na 100,000 za wanawake pamoja na pakiti 175,000 za mafuta ya kulainisha shughuli za miereka ya chumbani, katika siku 17 za Olimpiki za Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka 2016.Kwa mujibu wa ripoti kutoka Japan, kondomu hazitasambazwa kama mojawapo ya juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa hatari wa Covid-19 kupitia misuguano ya chumbani.“Pombe itaruhusiwa, lakini kila atakayekuwa na kiu ya ataikunywa katika chumba chake. Kondomu, ambazo zimekuwa zikisambazwa katika kila Olimpiki tangu Korea Kusini mwaka 1988, zitapeanwa tu wakati watu wakirejea makwao,” taarifa hizo zilisema.Washiriki watapimwa corona kila siku na lazima wavalie barakoa wakati wote “isipokuwa wakati wa kukula, kunywa ama kulala”.Mvunjaji wa masharti hayo na mengine mengi yaliyotangazwa Juni 20, atapigwa faini na kutupwa nje ya michezo hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Wajerumani walikosa kuongeza idadi 2020

Serikali yanyenyekea kuhusu amri kwa makanisa