• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Wakazi wa South Ngariama walalamikia hali mbovu ya barabara

Wakazi wa South Ngariama walalamikia hali mbovu ya barabara

Na SAMMY WAWERU

WAKAZI wa South Ngariama, Mwea, Kaunti ya Kirinyaga wanalalamikia miundomsingi duni ya barabara.

Kulingana na wenyeji, barabara eneo hilo zimeharibika kupita kiasi hali ambayo inatatiza shughuli za usafiri na uchukuzi.

Wengi wakitegemea shughuli za kilimo, wanasema msimu wa mvua huhangaika kupeleka mazao sokoni.

“Mvua inapokunya, barabara humu hazipitiki kwa sababu ya ubovu wake. Ni mahangaiko tupu,” mkulima Caroline Muriithi akaambia Taifa Leo.

Hali duni ya barabara, alisema huchangia mazao kuharibikia shambani.

“Hutatiza mpaka pikipiki, na ambazo hurahisisha shughuli za usafiri na uchukuzi,” mkazi huyo akasema, akilalamikia kukadiria hasara ya mazao msimu wa mvua.

Bi Anne Waiguru ndiye gavana wa Kaunti ya Kirinyaga. “Tumekuwa tukiihimiza serikali ya kaunti ituimarishie hali ya barabara za mashinani, ila kilio chetu hakiskiki,” akasema mkazi mwingine.

South Ngariama inafahamika katika ukuzaji wa mpunga, matunda kama vile ndizi, matikitimaji, mapapai na karakara.

Vile vile eneo hilo ni maarufu katika kilimo cha nyanya, mboga, mahindi na maharagwe. Pia hukuza miraa.

You can share this post!

Braut Haaland si wa kuuzwa hivi karibuni – Borussia...

Wanahandiboli Cereals Board na Nairobi Water mawindoni...