• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Wataalam, wanafunzi chini ya mwavuli wa MKU HSA washirikiana na kanisa kuwahudumia wakongwe mjini Machakos

Wataalam, wanafunzi chini ya mwavuli wa MKU HSA washirikiana na kanisa kuwahudumia wakongwe mjini Machakos

NA LAWRENCE ONGARO

WANAFUNZI wa kitengo cha afya katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya na kanisa la ACK kwa ushirikiano na wataalam, wametoa matibabu kwa wakazi wa kijiji cha Mitihani katika Kaunti ya Machakos.

Wanafunzi wa chama cha MKU Health Students Association (MKU HSA) na wadau katika kanisa la ACK Church-Mother Union walitoa huduma muhimu za afya kwa wakongwe zaidi ya 300.

Kulingana na afisa wa afya Ahmed Shenga zoezi hilo lilijumuisha kikundi cha madaktari, wahudumu wa afya wakiwemo wakufunzi bingwa na maafisa wengine wa kujitolea.

Zoezi hilo la siku moja lilishughulikia maradhi tofauti kama kisukari, malaria, kuharisha, damu kuchemka, viungo vya miwili,  na mengine mengi.

Wataalam, wanafunzi chini ya mwavuli wa MKU HSA washirikiana na kanisa kuwahudumia wakongwe mjini Machakos. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Afisa huyo wa afya Bw Shenga aliyeongoza hafla hiyo alikokuwa na kikundi cha kupima saratani, macho na maradhi mengine yanayohitaji uchunguzi zaidi, alisema ameridhishwa na namna shughuli ilivyoendelea.

“Tumechukua muda wetu mwingi kukagua wagonjwa wengi waliofurika eneo hili kutafuta matibabu,” alisema Shenga.

Alisema wakongwe wengi walinufaika na zoezi hilo ambapo wengi walisafirishwa na pikipiki kutoka sehemu za mbali ili kutafuta matibabu kamili.

Kanisa kuu la ACK-Mother Union lilitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo la Mitihani kwa kuletewa usaidizi wa kiafya kijijini.

Kitengo cha afya cha MKU kimeeleza ya kwamba kimebuni mpango kabambe wa kushirikiana na kanisa hilo ili kuwatibu wakazi wa kijiji hicho na hata katika maeneo mengine.

Dkt Josphat Njuguna anayesimamia kitengo cha afya MKU alisema hatua waliyochukua ni muhimu sana kwa sababu wamebadilisha maisha ya wengi katika kijiji hicho cha Mitihani.

Dkt Michael Mungoma wa kitengo cha dawa katika chuo hicho alishukuru ushirikiano uliopo kati yao na kanisa huku akisema utabadilisha maisha ya wakazi hao pakubwa.

Alitaja zoezi hilo kama la kufana kwa sababu wagonjwa wote waliofika walipata matibabu na dawa za bure.
  • Tags

You can share this post!

Azimio yawasilisha kwa mkuu wa polisi Nairobi barua ya...

Azimio wapeleka notisi ya maandamano ya wiki ijayo kwa mkuu...

T L