• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Watahiniwa watasaidiwa kusafiri – Oguna

Watahiniwa watasaidiwa kusafiri – Oguna

Na MARY WANGARI

WIZARA za Elimu na Usalama, zimeweka mikakati kabambe ya kuwezesha watahiniwa walionza mtihani ya KCSE Ijumaa, kurejea makwao salama licha ya marufuku ya kutoingia kaunti za Nairobi, Machakos, Kiambu, Kajiado na Nakuru.

Msemaji wa serikali, Kanali (Mstaafu) Cyrus Oguna aliwataka wazazi wasiwe na hofu kuhusu watoto wao.

“Hawapaswi kuwa na hofu kamwe. Wizara za Elimu na Usalama wa Nchi zina mpango madhubuti wa kuhakikisha wanafunzi wote ambao kwa sasa wanafanya mithani yao watafika makwao salama.

“Ujumbe wangu kwa wazazi ni kuwa, tunafahamu wanachopitia na tunafuatilia kwa makini jinsi watahiniwa wetu wanavyoendelea,” alisema Bw Oguna.

Alifafanua kuwa, taasisi za elimu zitashirikiana na Wizara za Elimu na Usalama kuhakikisha wanafunzi wanasafiri salama nyumbani kwao baada ya kukamilisha mtihani wao.

Mtihani wa KCSE ulioanza Ijumaa umepangiwa kukamilika mnamo Aprili 21, 2021.

You can share this post!

Aina hatari zaidi ya corona yagunduliwa TZ

Majambazi 5 sugu wauawa Mombasa