• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Watano wakana wizi wa pikipiki

Watano wakana wizi wa pikipiki

Na RICHARD MUMNGUTI

WASHUKIWA watano wanaodaiwa kuwa wanachama wa genge linaloiba pikipiki almaarufu Bodaboda na kuziuza eneo la kaskazini mwa Kenya na nchini Ethiopia wameshtakiwa.

Mabw Jibril Hassan Edin, Isaac Hassan Ibrahim, Rooney Jahwan Elisha, Kelvin Omboke Otieno na Stephen Munga walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Renee Kitangwa.Watano hao wanashtakiwa kwa kula njama za kuiba na wizi wa pikipiki.

Watano hao walikabiliwa na shtaka la wizi wa piki piki 169 kutoka kwa kampuni Mugo Auto Limited kati ya Januari na Septemba 2021. Shtaka lingine lilisema kuwa walikula njama za kutenda uhalifu wakishirikiana na watu wengine ambao hawakushtakiwa.

Mahakama ilifahamishwa idara ya uchunguzi wa jinai iliumbua sakata ambapo piki piki zilizoibwa kutoka Nairobi na Nyanza ziliuzwa mahala kwingine. Edin alitiwa nguvuni mnamo Oktoba 6,2021 katika duka lake mtaani Eastleigh ilhali Ibrahim alikamatwa katika kaunti ndogo ya Moyale mnamo Oktoba 9.

Edin anadaiwa amekuwa akiwashawishi wenye bodaboda kuchukua mikopo ya kununua piki piki kisha wailipe na mwaka mmoja. Anasemekana amekuwa akiwapa waendeshaji bodaboda Sh15,000.

Pia anadaiwa alikuwa anawapa wanaopeleka piki piki Sh10,000. Otieno, ambaye ni mekanika anashukiwa amekuwa akizibomoa piki piki na kutoa nambari za usajili. Alishtakiwa kupatikana na mali ya wizi pamoja na Munga katika kijiji cha Kiusyani kaunti ya Machakos.

Ibrahim alidaiwa alipatikana na piki piki na 361 nambari feki za usajili nyumbani kwake. Edin, Munga, Elisha na Otieno walikabiliwa na shtaka la kupatikana na piki piki za wizi maeneo ya Langata Nairobi na Machakos  Septemba 27 na Oktoba 3,2021.

Ibrahim pia ameshtakiwa kupatikana na piki piki zinazodhaniwa zilliibwa katika kaunti ndogo ya Moyale.

  • Tags

You can share this post!

360 Media FC ni mabingwa wa Nairobi West Regional League...

Mashabiki wataka Mwendwa achunguzwe vikali

T L