• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Wazee wa Mulembe wadai Ruto aliwaahidi urais akiondoka 2032

Wazee wa Mulembe wadai Ruto aliwaahidi urais akiondoka 2032

Na SHABAN MAKOKHA

Imeibuka kuwa viongozi kutoka jamii ya Waluhya walikubali kumuunga mkono Rais William Ruto na serikali yake ya Kenya Kwanza baada ya kuahidi kumuunga mkono mmoja wao kumrithi 2032.

Wiki jana Rais alipiga kambi katika eneo hilo ambapo alikutana na viongozi na makundi mbalimbali kutoka eneo la Magharibi kati ya Agosti 27 na Agosti 30 na kuzindua miradi ya maendeleo.

Viongozi wa kisiasa kutoka eneo hili wakiongozwa na magavana Paul Otuoma (Busia), Fernandes Barasa (Kakamega), Kenneth Lusaka (Bungoma) na Wilbur Ottichilo (Vihiga) waliandamana na Rais alipokuwa akizuru kaunti tano za magharibi  na kuahidi  kuunga mkono ajenda yake ya kuleta mabadiliko.

Kando na Bw Lusaka wa Bungoma (Ford Kenya) na George Natembeya wa Trans Nzoia (DAP-K), magavana hao wengine watatu walichaguliwa kwa tikiti ya ODM chini ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.

Mkuu wa Waziri Musalia Mudavadi na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula wanaotoka eneo hilo wanajiandaa kujitosa katika siasa za urithi za Kenya Kwanza mwaka wa 2032.

Bw Khalwale alisema Waluhya wataunga mkono serikali ya Kenya Kwanza hadi 2032 ili eneo hili linufaike na miradi ya maendeleo kama maeneo mengine ya nchi.

Alisema wakati wa mazungumzo yao, Dkt Ruto aliahidi kumuunga mkono kiongozi kutoka jamii ya Mulembe kumrithi muda wake utakapokamilika katika Ikulu.

“Tuliomba watu wetu wamuunge mkono William Ruto kwa sababu tulijua ataleta maendeleo katika eneo hili na ana ufunguo wa kufanya mluhya kuwa rais. Tunatarajia hili kufikia 2032,” akasema Bw Khalwale.

Magavana walisema uchumi wa nchi unaweza kuimarika na kustawi ikiwa viongozi wataungana na kufanya kazi kufufua uchumi uliodorora.

“Wakenya wanatutazama kama viongozi wao ili kuboresha maisha yao. Ufufuzi wa uchumi wetu haujui tofauti za kisiasa tulizo nazo kama Azimio au Kenya Kwanza. Kwa hivyo, tutamuunga mkono Rais na kumsaidia kuliongoza taifa kupata uhuru wa kiuchumi,” akasema Bw Barasa.

Bw Khalwale alisema Rais tayari amechagua timu ya watu wanaomsaidia kuunganisha viongozi wake wa Magharibi  kuekelea 2027 huku akitayarisha eneo hilo kumrithi 2032.

 

  • Tags

You can share this post!

Meli ya chakula cha msaada yawasili bandarini Lamu

Kongamano kuu la ACS23 lakamilika wito ukitolewa kwa...

T L