• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Wizara yakosa kutaja hesabu kamili ya fedha zilizotumika kufufua mpango wa 4K-Club

Wizara yakosa kutaja hesabu kamili ya fedha zilizotumika kufufua mpango wa 4K-Club

Na SAMMY WAWERU

WAZIRI msaidizi katika Wizara ya Kilimo Anne Nyaga amesema wizara yake haina hesabu kamili ya fedha zilizotumika kufufua mpango wa 4K-Club.

Juni 4, 2021 Rais Uhuru Kenyatta alizindua upya mpango huo wa mafunzo ya kilimo na ufugaji, ili kuanza kutekelezwa katika shule za msingi na upili nchini.

4K-Club ilikuwa maarufu na yenye mchango mkubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji chini ya utawala wa Rais (Mstaafu) Daniel Arap Moi, ambaye kwa sasa ni marehemu.

Waziri Anne amesema wizara yake haina takwimu kamili za kiwango cha fedha zilizotumika kufufua mpango huo, kwa kile ametaja kama “kuendelea kupata msaada kutoka kwa wadau husika”.

“Tunaendelea kupata msaada kutoka kwa mashirika na wadau husika,” akasema.

“Hatuna hesabu kamili ya kiwango cha fedha zilizotumika kufufua 4K-Club kwa sababu wafadhili wanaendelea kutupiga jeki, hususan nyanja tunazolenga,” Bi Anne akaelezea.

Kulingana naye, Wizara ya Kilimo inalenga kuhamasisha walimu ili wakumbatie utekelezaji wa 4K-Club.

Aidha, mpango huo unalenga kunoa vipaji katika sekta ya kilimo na ufugaji, hasa wakiwa shuleni.

Hatua hiyo ikisifiwa itasaidia kuboresha kilimo-ufugaji nchini, wadauhusika wanasema pia itachangia kuangazia kero ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana siku za usoni.

Mbali na kushiriki ukuzaji wa mimea na ufugaji, usafirishaji wa mazao, soko na uongezaji thamani ni nyanja zinazotajwa kusaidia kubuni nafasi za kazi.

You can share this post!

Omanyala atinga nusu-fainali ya mbio za mita 100 Olimpiki

Kaunti 10 za Mt Kenya kuondoa ada za biashara