• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Omanyala atinga nusu-fainali ya mbio za mita 100 Olimpiki

Omanyala atinga nusu-fainali ya mbio za mita 100 Olimpiki

Na GEOFFREY ANENE

MSHIKILIZI wa rekodi ya kitaifa ya mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala Omurwa amefuzu kushiriki nusu-fainali kwenye Olimpiki baada ya kukamilisha kundi lake katika nafasi ya tatu jijini Tokyo, Japan mnamo Julai 31.

Omanyala aliyeingia mbio hizo akiorodheshwa katika nafasi ya 68 duniani kwa sekunde 10.01, alikamilisha umbali huo kwa muda uo huo nyuma ya mshindi Andre de Grasse kutoka Canada (9.91) na Mwamerika Fred Kerley (9.97).

Kerley (9.86) na De Grasse (9.99) walikuwa na kasi bora kuliko Mkenya huyo kabla ya mbio hizo.

Wengine walioshiriki mchujo huo wa kundi la tano ni Divine Oduduru (10.05), Muingereza Reece Prescod (10.13), Mwitaliano Filippo Tortu (10.17), Mturuki Jak Ali Harvey (10.27), raia wa Oman, Barakat Al Harthi (10.27) na Mohamed Alhammadi (10.59).

Hata hivyo, Oduduro alilishwa kadi nyekundu kwa kuanza mapema.

Wakimbiaji watatu-bora kutoka makundi yote saba pamoja na watatu waliomaliza nje ya nafasi hizo za muda mzuri walitinga nusu-fainali itakayofanyika Agosti 1.

You can share this post!

Mbinu za kuzima Ruto Mlimani zaanza kusukwa

Wizara yakosa kutaja hesabu kamili ya fedha zilizotumika...