• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Afisa aliyetumia cheti feki kupanda cheo atupwa jela

Afisa aliyetumia cheti feki kupanda cheo atupwa jela

Na VITALIS KIMUTAI

TUME ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) imempata mfanyakazi wa serikali ya Kaunti ya Bomet na hatia ya kughushi stakabadhi zake za masomo ambazo alizitumia kutuma maombi ya kupandishwa ngazi.

Kutokana na kosa hilo, mfanyakazi huyo, aliyetambuliwa kama Bw Dennis Yegon, alipigwa faini ya Sh900,000.

Ikiwa atashindwa kulipa faini hiyo, basi atafungwa gerezani kwa mwaka mmoja.Jumanne, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kericho, Samuel Mokua, alitoa adhabu hiyo kwa mshtakiwa kutokana na kosa hilo analodaiwa kufanya mnamo Julai 31, 2018.

Bw Yegon anahudumu katika Idara ya Kutoa Kandarasi.Kwenye mashtaka yaliyowasilishwa na EACC, Bw Yegon alidaiwa kutumia stakabadhi hizo kutuma ombi la kuteuliwa kama Mkurugenzi wa Idara ya Utoaji Kandarasi.

Nafasi hiyo ilitangazwa na Bodi ya Uajiri ya Kaunti (PSB) mnamo Februari 14, 2018, ambapo alikuwa miongoni mwa watu wanne ambao waliorodheshwa na kuhojiwa kuhusu nafasi hiyo.

Alikabiliwa na mashtaka sita ya kuwasilisha stakabadhi ghushi, kughushi stakabadhi za elimu na kutoa maelezo ya uwongo.

“Imedhihirishwa mbele ya mahakama hii kwamba vyeti vya Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE), Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE), shahada ya kwanza na masuala ya tarakilishi vilikuwa vya kweli,” akasema Bw Mokua.

Hata hivyo, cheti cha shahada ya uzamili alichowasilisha kwa bodi hiyo ni ghushi.

“Chuo Kikuu cha Egerton kilisema hakikuwa kikitoa mafunzo ya shahada ya uzamili kuhusu Masuala ya Usimamizi wa Biashara (MBA) wakati mshtakiwa alipowasilisha cheti chake,” akasema Bw Mokua.

“Chuo Kikuu cha Egerton kilisema hakikuwa kikitoa mafunzo ya shahada ya uzamili kuhusu Masuala ya Usimamizi wa Biashara (MBA) wakati mshtakiwa alipowasilisha cheti chake,” akasema Bw Mokua.

Kulingana na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Mstaafu Joshua Teter, Afisa Mkuu Mtendaji na Katibu wa Bodi Philip Tonui, stakabadhi alizowasilisha mshtakuwa zilikuwa za kweli.

Wawili hao waliiambia mahakama kwamba Bw Yegon ndiye aliibuka bora kwenye mahojiano hayo, na angeteuliwa ikiwa EACC haingefichua uhalali wa cheti cha shahada yake ya uzamili.

Alama za mahojiano ambazo watu hao wanne walipata ziliwasilishwa mbele ya mahakama.

Ili kutolea maoni habari hii, nenda kwa taifaleo.nation.co.ke

You can share this post!

Bayern Munich wasubiri hadi dakika za mwisho kusambaratisha...

Waiguru asifu Ajenda Kuu Nne za Rais Kenyatta akisema...

T L