• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Serikali kuokoa wanyamapori ili wasiangamizwe na ukame

Serikali kuokoa wanyamapori ili wasiangamizwe na ukame

Na MACHARIA MWANGI

SERIKALI imehofishwa na hali ya kiangazi katika baadhi ya sehemu za nchi ambayo imewaathiri hata wanyamapori.

Akizungumza Jumapili akiwa mjini Naivasha, Waziri wa Utalii Najib Balala alisema wanafanya mipango ya kuwapelekea maji wanyama hao. Alisisitiza haja ya kuwatunza wanyamapori akiwataja kama urithi wa taifa.

“Tumeshiriki mazungumzo katika kiwango cha Baraza La Mawaziri na ni wazi pana haja ya kuwatunza binadamu pamoja na wanyamapori,” alisema.

Alitoa wito kwa Taasisi mpya ya Utafiti na Mafunzo kuhusu Wanyamapori (WRTI) kubuni suluhisho thabiti za kuzuia athari za mabadiliko ya hali ya anga na ukame.

Bw Balala alitaja mzozo baina ya binadamu na wanyamapori kama changamoto kuu inayokabili sekta hiyo akikiri kuwa wameweza kudhibiti visa vya uwindaji haramu vilivyokithiri.

“Mwaka huu, Wizara imetengewa Sh500 milioni na Hazina ya Kitaifa lakini bado tuna malimbikizi ya kuanzia 2014 hadi 2020, ambayo ni karibu Sh13 billion,” alifichua waziri.

You can share this post!

Ziara ya Raila yafufua uhasama wa Kiraitu, Munya

Mshukiwa wa tatu katika mauaji ya Tirop anyakwa

T L