• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Azimio wamponda balozi wa Amerika

Azimio wamponda balozi wa Amerika

NA CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga amemkaripia vikali balozi wa Amerika nchini Kenya, Meg Whitman kwa kuhalalisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Akiongea jana Alhamisi katika Kongamano la Ugatuzi mjini Eldoret, Bw Odinga alitisha kuanzisha kampeni ya kushinikiza balozi huyo arejeshwe nchini mwao kwa “kuingilia masuala ya ndani ya Kenya.”

Bw Odinga pia ametetea maandamano akisema ndio yalichangia kupatikana kwa Katiba ya sasa iliyoanzisha utawala wa ugatuzi na kuundwa kwa Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (NDC) ya kuleta maridhiano ya kisiasa nchini.

Huku akimtaja Bi Whitman kama “balozi mtundu” Bw Odinga alimwonya dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Kenya kwani ni nchi huru.

“Ningependa kumwambia yule balozi mtundu kwamba Kenya sio Amerika. Kenya sio koloni ya Amerika, fyata mdomo wake la sivyo tushinikiza urejeshwe nchini mwako,” Bw Odinga akasema bila kumtaja balozi huyo kwa jina.

Tishio lake lilipokelewa lilipolewa kwa shangwe na baadhi ya wajumbe waliokuwemo katika ukumbi wa Eldoret Sports Club.

Miongoni mwa vigogo wa Azimio walioandamana na Bw Odinga ni pamoja na magavana wa zamani Wycliffe Oparanya (Kakamega), Mwangi wa Iria (Murang’a), kingozi wa chama cha DAP-Kenya Eugene Wamalwa na kiongozi wa chama cha Roots Profesa George Wajackoyah.

Akiongea Jumatano wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa kongamano hilo, balozi Whitman alisema kuidhinishwa kwa matokeo ya urais na Mahakama ya Juu kulikuwa ni ithabati kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa njia huru na haki.

“Uchaguzi wa urais wa 2022 ulikuwa wa haki zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya Kenya na matokeo yaliidhinishwa na Mahakama ya Juu. Na baadaye mamlaka yalipitishwa kwa kiongozi mpya kwa amani,” akasema huku akishangiliwa na waliokuwemo akiwamo Rais William Ruto.

Balozi huyo alikariri kuwa waangalizi wa uchaguzi wa humu nchini na wale wa kimataifa pia walikubaliana na matokeo ya uchaguzi huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Bi Whitman kusifu namna uchaguzi huo wa Agosti 9, 2022 na kukubali ushindi wa Rais Ruto aliyezoa kura 7.1 milioni huku Odinga alipata kura 6.9 milioni.

Hata hivyo, Bw Odinga na vigogo wenza wa Azimio wamepinga matokeo hayo wakiamini matokeo ya mfichuzi fulani aliyedai Bw Odinga alipata kura 8.1 milioni.

Awali, maseneta wa Azimio pia walimshutumu Whitman wakisema ni “mapema kwake kuidhinisha matokeo ya urais ya 2022.”

Wakiongozwa na Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang walisema balozi huyo hakufaa kutoa kauli hiyo kwa sababu matakwa ya Azimio kwamba matokeo ya uchaguzi wa urais yakaguliwe hayajatimizwa.

“Sio sawa kwa balozi wa Amerika Whitman kuwa uchaguzi wa urais uliendeshwa kwa njia ya huru na haki ilhali sava ya IEBC haijafunguliwa ili ikaguliwe kuthibitisha mshindi halisi wa uchaguzi wa urais. Hili mojawapo ya masuala ambayo tumewasilisha mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo ili kutuliza joto la kisiasa nchini,” akawaambia wanahabari katika ukumbi wa Eldoret Sports Club.

“Kwa hivyo, ni mapema kwa Balozi Whitman kutoa kauli kama hiyo wakati kama huu kwani huenda ikahujumu malengo ya mazungumzo hayo,” Bw Kajwang’ akasema. Kinaya ni kuwa balozi huyu ni miongoni mw mabalozi wa mataifa ya magharibi ambao wamekuwa wakihimiza mazungumzo baina ya mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio kuleta maridhiano ya kisiasa nchini.

Jana Jumatano, Bw Odinga pia alitetea maandanamo ambayo aliitisha kushinikiza ukaguzi wa mitambo ya kunakili matokeo ya kura za urais, miongoni mwa matakwa mengine.

“Kabla ya kuketi ningependa kumwambia gavana Jonathan Bii kwamba Katiba hii ni zao la maandamano. Mandamano ndio yamesababisha Ichung’wah na Kalonzo kuketi katika meza ya mazungumzo,” akasema.

Bii Bii alikuwa amekejeli maandamano ya Azimio akisema kuwa wao kama wakazi wa Uasin Gishu waliyapuuza na kuelekeza juhudi zao shambani na ndipo watapata mavuna mazuri msimu huu.

“Huku ninyi mkiandamana barabarani kwa kuweka sufuria vichwani, sisi hapa tuliandamana mashambani na sasa tutavuna chakula kwa wingi,” akasema.

MASENETA

Awali maseneta wa Muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya walimkemea Balozi Whitman kwa kudai kuwa uchaguzi mkuu wa 2022 ulioendeshwa kwa njia huru na haki.

Wakiongozwa na Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang maseneta hao Alhamisi walisema kuwa balozi huyo hakufaa kutoa kauli hiyo kwa sababu matakwa ya Azimio kwamba matokeo ya uchaguzi wa urais yakaguliwe hayajatimizwa.

“Sio sawa kwa balozi wa Amerika Whitman kuwa uchaguzi wa urais uliendeshwa kwa njia ya huru na haki ilhali sava ya IEBC haijafunguliwa ili ikaguliwe kuthibitisha mshindi halisi wa uchaguzi wa urais. Hii mojawapo ya masuala ambayo tumewasilisha mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo ili kutuliza joto la kisiasa nchini,” akasema katika ukumbi wa Eldoret Sports Club mjini Eldoret ambako Kongamano la Ugatuzi.

“Kwa hivyo, ni mapema kwa Balozi Whitman kutoa kauli kama hiyo wakati kama huu ambapo sote tumejitolea kuunga mkono mchakato wa mazungumzo,” Bw Kajwang’ akasema.

Alikuwa ameandamana na mwenzake, Mohammed Faki (Mombasa), Eddy Oketch (Migori), Okong’o Omogeni (Nyamira) Oburu Oginga (Siaya) na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna.

Maseneta hao pia walimkashifu balozi Whitman kwa kuisifu serikali ya Kenya Kwanza kwa kuimarisha vita dhidi ya ufisadi, wakisema hiyo hiyo sio kweli. Aidha, walimshutumu balozi huyo kwa kuunga mkono viwango ushuru ambavyo vimendekezwa

Akiongeza Jumatano wakati wa kufunguliwa rasmi kwa kongamano hilo la ugatuzi balozi Whitman alisema uchaguzi mkuu uliopita haswa ule wa urais uliendeshwa kwa njia huru na haki.

“Uchaguzi mkuu wa 2022 ulikuwa uchaguzi ambao matokeo yake yaliaminika zaidi katika historia ya Kenya na matokeo yake yalithibitishwa na Mahakama ya Juu. Aidha, upitishwaji wa mamlaka ulifanyika kwa njia ya amani,” akasema Bi Whitman katika hafla hiyo iliyoongozwa na Rais William Ruto.

Balozi huyo ambaye aliletwa nchini mnamo Februari mwaka jana, pia alipongeza serikali ya Dkt Ruto katika vita vyake dhidi ya ufisadi.

Alisema hata ingawa serikali imepiga hatua katika vita hivyo, juhudi zaidi zinapasa kuongezwa kwa sababu uovu huo unahujumu ari ya Wakenya kushiriki katika masuala ya maendeleo na uwezekezaji.

“Rais Wiliam Ruto amelaani ufisadi kwa kukaripia mashirika ya serikali yanayoajiri watu wenye maadili mabaya. Wakome kufanya hivyo. Kwa kufuta kazi maafisa waliotajwa katika sakata za ufisadi, hiyo itakuwa hatua nzuri. Lakini mengi yanafaa kufanywa ili kudhibiti uovu huo,” Bi Whitman akasema.

Aidha, balozi huyo pia alisema viwango vya ushuru nchini havifaa kuwa chini zaidi bali ushuru ambao unaweza kutegemewa.

“Sheria ya Fedha iliyopitishwa juzi yalileta mabadiliko mengi ambayo yatachukua muda wa miaka 10 kuhakikisha kuwa mfumo wa ushuru ni wa kutegemewa. Aidha, sera za ushuru zinapasa kuvutia wawekezaji,” akasema Balozi Whitman.

Hata hivyo, balozi huyo aliisifu Kenya kwa kuitaja kama  kuwa kitovu bora cha uwekezaji

  • Tags

You can share this post!

Huenda Mandago alichokoza nyuki kabla ya kukamatwa kwake,...

Ruweida Obo ataka fidia ilipwe kwa wanaouawa au kujeruhiwa...

T L