• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Familia ya Tob Cohen haitaki aliyekuwa mkewe akijitambua kwa jina la marehemu

Familia ya Tob Cohen haitaki aliyekuwa mkewe akijitambua kwa jina la marehemu

Na RICHARD MUNGUTI

FAMILIA ya raia wa Uholanzi Tob Cohen aliyeuawa na maiti yake ikatupwa ndani ya shimo la choo katika makazi yake mtaa wa kifahari wa Kitsuru inaomba mahakama imzuilie mkewe Sarah Wairimu Kamotho akitumia jina la marehemu kudai mali.

“Sarah hapasi kujitambua kwa jina Sarah Wairimu Kamotho Cohen….kwa vile hakuwa ameolewa rasmi na marehemu,” tumia jina la Cohen kudai,” wakili Danstan Omari alimweleza Jaji Mugure Thande. Jaji Thande ameombwa na Bi Gabrieli Van Straten, dada yake marehemu asimruhusu atumie jina la Cohen kudai urithi katika mali ya mwenda zake.

Mahakama imeelezwa kuwa Cohen alipokuwa hai Sarah Wairimu alikataa kubadilisha jina lake kujitambulisha kwa jina mumewe marehemu. “Wairimu hakubadilisha jina lake alipoolewa kujitambua kama mke wa marehemu Tob Cohen. Hakubadilisha jina kutambuliwa kwa jina la “Cohen”.

Hivi basi sasa hawezi ruhusiwa kubandika jina la Cohen katika majina yake-Sarah Wairimu Kamotho Cohen,” asema Garbriella Gabriel. Wakili Omari anaomba mahakama kuu itupilie mbali kesi zote alizoshtaki Sarah akijitambua kwa jina Sarah Wairimu Cohen.

Mahakama imeelezwa Sarah anajaribu kutumia ujanja ajifaidi na mali ya marehemu kwa njia ya ulaghai. “Kesi zote alizowasilisha Sarah zapasa kutupiliwa mbali kwa vile hatambalikani kisheria kuwa mke wa Tob Cohen,” ushahidi aliowasilisha kortini Gabriella wadokeza.

Sarah anakabiliwa na shtaka la kumuua kinyama Tob Cohen na kutupa mwili wake ndani ya shimo la choo katika makazi yao katika mtaa wa kifahari wa Kitsuru. Gabriella anasema uhusiano kati ya Wairimu na nduguye marehemu ulikuwa umedorora.

Marehemu alikuwa ameanza kesi watenganishwe na Wairimu lakini akauawa kinyama. Gabriella anasema kuwa Wairimu anataka aonewe huruma kama mjane lakini anaomba korti isiponyokwe na ukweli kwamba Wairimu ameshtakiwa kumuua mumewe.

“Tob Cohen alipokuwa hai Sarah alikataa akitambulishwa kuwa mke wake lakini sasa anataka atambuliwe mautini,” dada yake marehemu anadokeza. Haya yanajiri kufuatia agizo la Jaji Thande wosia mbili zilizopo kuhusu umiliki wa mali ya Cohen ziwasilishwe kortini.

Familia ya Cohen ilikabidhiwa Wosia alioacha ameandika na wakili Chege Kirundi. Sarah Wairimu pia yuko na wosia wake. Wosia hizi mbili zitawasilishwa kortini ili ile ya ukweli ibainike. Mahakama imetoa agizo mali yake Cohen isigawanyishwe ama kuuzwa hadi kesi ya umiliki wa mali yake isikizwe na kuamuliwa.

You can share this post!

Wanjigi alala ndani licha ya kujifungia usiku kucha

Tiba asili

T L