• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Kenya Power kuanza kutoa umeme kwa vipimo ili usipotee mara kwa mara

Kenya Power kuanza kutoa umeme kwa vipimo ili usipotee mara kwa mara

JOHN MUTUA NA MARY WANGARI

KAMPUNI ya Kenya Power itaanza kusambaza umeme kwa vipimo, ikilenga eneo la Magharibi katika jitihada za kupunguza presha kwenye laini kuu ya umeme ambayo imekuwa ikishindwa kuhimili ongezeko la mahitaji.

Waziri wa Kawi Davis Chirchir jana alisema kuwa wizara hiyo imetafuta suluhu ya muda mfupi kutokana na kukatika kwa umeme kote nchini ambako kulikumba taifa Jumapili jioni.

Kenya ilikumbwa na hitilafu ya umeme kote nchini kuanzia saa moja na nusu Jumapili usiku, baada ya laini ya Kisumu-Muhoroni iliyotumika kupita kiasi kukwama.

Mgao wa umeme katika nchi nyingi unasababishwa na uzalishaji duni wa umeme ambao unashindwa kukidhi mahitaji kama ilivyo nchini Afrika Kusini na mataifa jirani.

Hatua ya Kenya Power itaudhi wawekezaji katika eneo la Magharibi kwa kuongeza gharama zao za kuendesha biashara huku ikifanya laini kuu ya kusambaza umeme ambayo haijafanyiwa marekebisho kwa miaka mingi kupigwa darubini.

Alisema shinikizo kuu kupita kiasi kwenye laini ya kusambaza stima ya Kisumu- Muhoroni ndicho kiini cha stima kupotea kote nchini mnamo Jumapili.

Soma pia: https://taifaleo.nation.co.ke/makala/kenya-power-yakashifiwa-kwa-utepetevu-taifa-likikosa-stima-kwa-mara-ya-tatu

Laini hii husambaza umeme katika maeneo ya Magharibi, Nyanza Kusini na maeneo ya Kusini mwa Bonde la Ufa.

Huku akifichua kwamba ukarabati wa mifumo ya umeme nchini haujafanyika kwa muda wa miaka sita iliyopita, Waziri alisema serikali kupitia ufadhili wa serikali ya Japan na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) inapanga kujenga mtandao mpya kati ya Narok na Bomet.

Wakati uo huo, Seneta wa Nandi Samson Cherargei sasa anaitaka Kampuni ya Kusambaza Umeme (KPLC) kuwafidia Wakenya kwa hasara waliyopata kutokana na stima kupotea kila mara hivi majuzi.

Akihutubia vyombo vya habari katika majengo ya Bunge, Seneta huyo amesema wakati umewadia kwa taifa kuwa na mdahalo kuhusu kumaliza ukiritimba wa KPLC ambayo imekuwa kero.

  • Tags

You can share this post!

Mlinzi ashtakiwa kuiba gia za kuteremsha jeneza kaburini

Nimeolewa na mume mzuri, lakini ujuzi wa ex wangu kwenye...

T L