• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 10:18 AM
Kidero akosa kufika kortini, aenda Kasarani

Kidero akosa kufika kortini, aenda Kasarani

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Dkt Evans Kidero anayekabiliwa na kesi ya ufisadi kuhusu Sh68 milioni jana alihudhuria hafla ya Azimio la Umoja katika uwanja wa Kasarani badala ya kufika kortini kesi hiyo ilipotajwa.

Mbali na Dkt Kidero, wakili James Orengo anayemwakilisha pia hakufika kortini baada ya kuhudhuria hafla hiyo.Bw Orengo alimtuma wakili Aulo Soweto kueleza hakimu mkuu Felix Kombo hawatafika kortini.Hata hivyo, Bw Kombo alisema kesi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kutajwa washtakiwa kuifahamisha mahakama ikiwa wamekabidhiwa nakala za mashahidi.

Bi Soweto alieleza mahakama kuwa, upande wa mashtaka haujawakabidhi nakala zote za mashahidi.“Tumepewa nakala chache za ushahidi. Bado zijapokea nakala muhimu nne,” alisema Bi Soweto.Pia, Bi Soweto alisema kuna ushahidi ambao upande wa mashtaka umekataa nao na kusema “hawatawapa.”

Kiongozi wa mashtaka Bw James Kihara alieleza mahakama hajapokea barua ya malalamiko kutoka kwa Bi Soweto akieleza matatizo aliyokumbana nao.“Naomba Bi Soweto aandike barua akieleza ushahidi ambao hajapokea ndipo apewe,” alisema Bw Kihara.

Kidero ameshtakiwa kulipa kinyume cha sheria zaidi ya Sh68 milioni kutoka akaunti za kaunti ya Nairobi.Bw Kombo aliamuru Dkt Kidero akabidhiwe nakala zote za ushahidi na kuorodhesha kesi hiyo kutajwa Januari 21,2022.

You can share this post!

Wakazi wadaiwa kubadilisha dini ili kupata misaada

Korir na Cheptonui kuongoza Wakenya 12 Malaga Marathon

T L