• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:42 PM
Wakazi wadaiwa kubadilisha dini ili kupata misaada

Wakazi wadaiwa kubadilisha dini ili kupata misaada

Na MAUREEN ONGALA

BAADHI ya wakazi wa eneo la Dingiria katika eneobunge la Ganze, Kaunti ya Kilifi, wamedaiwa kubadilisha dini ili wanufaike na misaada ya chakula.

“Hali ya maisha katika eneo letu imekumbwa na changamoto nyingi kutokana na ukame. “Watu wengi hawana chakula na wanalazimika kubadili dini ili kupata msaada huo katika maeneo ya ibada,” akasema mkazi Bi Mary Safari.

Naibu Kamshina wa Ganze, Bw George Chege, hata hivyo alikanusha madai hayo. Naye diwani wa wadi ya Ganze, Bw Benson Chengo, alieleza kuwa hitaji la kubadilisha dini sio kigezo cha kuwasaidia watu maskini katika jamii.: “Ikiwa mkazi amejiunga na dini kwa sababu ya njaa ina maana kuwa hana imani na atatoka chakula kitakapopatikana kwa wingi.’

You can share this post!

Ulaghai ni kiini cha kutibua vita vya ufisadi – DPP

Kidero akosa kufika kortini, aenda Kasarani

T L