• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Mama wa Taifa avalia mavazi ya bei ghali siku ya Utamaduni

Mama wa Taifa avalia mavazi ya bei ghali siku ya Utamaduni

NA CHARLES WASONGA

SHEREHE za Kitaifa za Sikukuu ya Utamaduni Dei zimefanyika Jumanne, Oktoba 10, 2023, katika Ukumbi wa Bomas of Kenya na Mama wa Taifa, Rachel Ruto, ndiye amekuwa mgeni wa heshima.

Alimwakilisha Rais William Ruto ambaye wakati huu yuko nchini Uganda kwa ziara rasmi.

Mama Rachel alikuwa amevalia nguo ya kijani kibichi yenye virembesho vya maua vilivyoafiki sherehe hizo.

Aidha, alikuwa amevalia mshipi wa kipekee wa bei ghali chapa ‘Valentino Garavan belt’ wenye alama ya V na rangi ya dhahabu.

Kulingana na tovuti moja ya kuuza bidhaa, mshipi ambao Mama Rachel alikuwa amevalia unauzwa kwa si chini ya Sh85,000 nchini Kenya.

Itakumbukwa kwamba mnamo Agosti 2023, Rais Ruto alizuru Uganda kwa mkutano na Rais Yoweri Museveni.

Dkt Ruto alisema mazungumzo yake na Bw Museveni yalihusu masuala yenye manufaa kwa Kenya na Uganda, yakiwemo Biashara, Usalama na Kilimo.

Rais alikuwa amevalia suti nadhifu ya Kaunda ambayo ilivutia hisia za Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walipoona picha zilizotolewa na Ikulu na kusambazwa kwa vyombo vya habari.

Mkenya mmoja kwenye mtandao wa X alisema kuwa saa ya mkononi na viatu ambavyo Dkt Ruto alivalia ni vya bei ya juu zaidi.

Ilibainika alikuwa amevalia saa chapa ‘A Lange 1 Moon Phase watch’ ambayo bei yake ni kati ya Sh5 milioni hadi Sh12 milioni, kulingana na sifa za saa husika.

Aidha, Rais Ruto alikuwa amevalia jozi ya viatu vya thamani ya Sh128,000.

Mwezi Septemba wakati wa kisa ambapo nguvu za umeme zilipotea kote nchini na mitambo ya kuzalisha umeme mbadala katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) kufeli kufanya kazi, Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen alifika uwanjani humo kukagua hali akiwa amevalia jozi ya viatu vilivyokadiriwa kuwa vya thamani ya Sh103,000.

  • Tags

You can share this post!

Mgogoro Meru: Wapinzani wa Mwangaza sasa wageukiana

Obama akashifu Hamas kwa ‘shambulizi la kigaidi lenye...

T L