• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
Muwe makini na matokeo ya KCSE 2023 mkitaka tusiwashtaki, KUPPET yaambia KNEC na wizara

Muwe makini na matokeo ya KCSE 2023 mkitaka tusiwashtaki, KUPPET yaambia KNEC na wizara

NA ALEX KALAMA

MUUNGANO wa walimu wa shule za sekondari na vyuo vya kadri (Kuppet) tawi la Kilifi, umetishia kuelekea mahakamani iwapo matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE 2023), yatakuwa na dosari kama yale ya Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE 2023).

Akizungumza mjini Malindi, katibu mtendaji wa Kuppet tawi la Kilifi Bw Caleb Mogere ameeleza kuwa ni sharti Baraza la Mitihani Nchini (Knec) kusahihisha mitihani kwa uangalifu.

“Wanaposahihisha mitihani, na kunakili alama wafanye hivyo kwa njia bora na sawa na masomo ambayo mtahiniwa alifanya shuleni,” akasema Bw Mogere.

Katibu huyo vile vile ameitaka Wizara ya Elimu nchini kuhamisha itakayokuwa Gredi ya Nane na Gredi ya Tisa kutoka katika majengo ya shule za msingi na kuwa ndani ya shule za sekondari kutokana na miundomisingi ya kutosha inayopatikana katika shule hizo.

Hii ni baada ya Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu mnamo Jumatatu kuweka wazi kuwa wanafunzi hao watasalia katika majengo ya shule za msingi.

  • Tags

You can share this post!

Polisi anayetuhumiwa kumjeruhi mzee katika mzozo wa pombe...

Simbajike Wamuchomba akataa kuunga ripoti ya kumtengenezea...

T L