• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Simbajike Wamuchomba akataa kuunga ripoti ya kumtengenezea Raila ofisi ya mshahara

Simbajike Wamuchomba akataa kuunga ripoti ya kumtengenezea Raila ofisi ya mshahara

NA WANDERI KAMAU

MBUNGE wa Githunguri, Gathoni Wamuchomba, Jumatatu alisema kuwa hataunga mkono ripoti ya Kamati ya Mazungumzo ya Kitaifa (NADCO), akisema inalenga kumpa mamlaka kiongozi wa Azimio, Bw Raila Odinga, licha ya kutochaguliwa kama rais na Wakenya kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2023.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, Bi Wamuchomba alisema kuwa ni kinaya kwamba ripoti hiyo inapendekeza Bw Odinga kutengewa afisi ya Kiongozi Rasmi wa Upinzani, ilhali alishindwa na Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu.

Mojawapo ya mapendekezo makuu ya ripoti hiyo ni kubuniwa kwa Ofisi ya Kiongozi Rasmi wa Upinzani, ili kuhakikisha anaangalia na kufuatilia utendakazi wa serikali.

Wakenya wengi wamekuwa wakieleza kuwa Bw Odinga ndiye atakayefaidika kutokana na kubuniwa kwake.

“Moja ya sababu zilizowafanya watu wengi kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022, ni kuhakikisha kuwa Bw Odinga hakushinda urais. Ni vipi tena tunaambiwa kuunga mkono ripoti inayopendekeza atengenezewa afisi kubwa? Katika ofisi hiyo, atatengewa fedha za kuiendesha, atakuwa na wafanyakazi, mshahara na magari, ambapo gharama zote zitatokana na fedha za walipaushuru. Huko ni kuwarudisha nyuma Wakenya,” akasema Bi Wamuchomba.

Zaidi ya hayo, Bi Wamuchomba pia alidai kuwa baadhi ya wabunge kutoka ukanda wa Mlima Kenya wamekuwa wakiogopa kuishinikiza serikali ya Kenya Kwanza kutekeleza mpango wa Kura Moja-Shilingi Moja-Kura Moja, ili kutoonekana kama “waasi dhidi ya serikali”.

“Watu wetu wanateseka ila wabunge wengi wanaogopa kuikosoa serikali ili kutoonekana waasi. Binafsi, sitaogopa, kwani mfumo huo ndio pekee utakaowasaidia wakazi wa ukanda wa Mlima Kenya,” akasema mbunge huyo.

  • Tags

You can share this post!

Muwe makini na matokeo ya KCSE 2023 mkitaka tusiwashtaki,...

Shamrashamra: Usalama waimarishwa wageni wakifurika Pwani

T L