• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 12:31 PM
Ruto asema serikali itaanza kukopa mama mboga na wahudumu wa bodaboda pesa

Ruto asema serikali itaanza kukopa mama mboga na wahudumu wa bodaboda pesa

NA RICHARD MAOSI

RAIS William Ruto amesema serikali itaanza kutafuta mikopo kutoka kwa akaunti za Wakenya.

Wale ambao wamewekwa kwenye mpango wa kukopesha serikali ni mama mboga, mtu wa bodaboda na Mkenya yeyote yule mwenye kipato.

Dkt Ruto alitoa matamshi hayo mnamo Jumapili, Novemba 26, 2023, hilo likionekana kama mojawapo ya hatua kustawisha uchumi wa taifa bila kutegemea mikopo kutoka mataifa ya nje.

Kulingana na Rais, hivi sasa Kenya inategemea mikopo kutoka nje kwa sababu wakopeshaji wetu walitutangulia kwa kuweka akiba.

“Badala ya kusaka hela kutoka kwa wale ambao walijiwekea akiba mapema, tunataka kuweka akiba yetu ili tujitegee,”akasema kiongozi wa nchi.

Alisema Kenya inastahili kujifunza kutoka kwa nchi zilizoendelea, akisisitiza kwamba zimekuwa zikikopa pesa kutoka kwa wananchi wake.

Awali, Rais Ruto aliungama kuwa serikali ilikuwa ikilemewa na mzigo mzito wa madeni na kwamba haikuwa na akiba ya kutosha kujitosheleza, ndiposa bado taifa linategemea mikopo.

Akizungumza katika kanisa la Faith Evangelical Ministry, Karen Nairobi, Rais alisema miaka 10 hadi 15 ijayo, Kenya haitakuwa ikitegemea mikopo kutoka mataifa ya ng’ambo.

Julai 2023, Naibu Rais Rigathi Gachagua alihimiza Wakenya wajifunze namna ya kuweka akiba ili nchi isitegemee mikopo kutoka ughaibuni.

 

  • Tags

You can share this post!

Huzuni 1 akiuawa na nyumba 10 kuteketezwa moto kwenye...

Shule ya Moi Kabarak Nakuru yaendelea kuficha matokeo yake...

T L