• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Ruto: Ushuru tunaotoza wananchi umepunguzia nchi hatari ya madeni na mikopo

Ruto: Ushuru tunaotoza wananchi umepunguzia nchi hatari ya madeni na mikopo

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto ametetea mfumo wake wa utozaji ushuru (VAT), akidai umeondolea Kenya hatari ya madeni na mikopo.

Akihutubu Jumanne, Desemba 12 wakati wa maadhimisho ya Jamhuri Dei 2023, Dkt Ruto alisema nchi haipo katika hali iliyokuwa hapo awali ya mikopo.

“Taifa sasa halipo kwenye hatari ya madeni na mikopo kama ilivyokuwa hapo awali,” Rais akasema.

Rais Ruto aliongoza nchi kuadhimisha miaka 60 ya kujitawala, tangu Kenya ipate uhuru wa kujitawala Desemba 12, 2023.

Alitumia jukwaa la sherehe za Jamhuri Dei 2023 kupigia upatu serikali yake – Kenya Kwanza, akihoji mikakati aliyoweka imesaidia kukwamua nchi kutoka kwenye hatari ya madeni na mikopo.

Rais Ruto aidha aliashiria mfumo wa utozaji ushuru ambapo 2023 alipandisha VAT ya mafuta ya petroli kutoka asilimia 8 hadi 16.

Nyongeza hiyo ya ushuru imechochea gharama ya maisha kuwa ngumu.

Isitoshe, kuna ada za ushuru ambazo zimezinduliwa ikiwemo ile ya nyumba za bei nafuu.

Kenya inadaiwa zaidi ya Sh10 trilioni, madeni hayo yakiwa ni ya kigeni.

Kauli ya Rais Ruto inaonekana kama kinaya, ikizingatiwa kuwa serikali yake inaendelea kuchukua mikopo nje ya nchi.

Alipotwaa uongozi 2022 kutoka kwa mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta ambaye kwa sasa ni Rais Mstaafu, naibu wake, Bw Rigathi Gachagua alisema walirithi serikali iliyofilisika.

  • Tags

You can share this post!

Madai watu walilipwa kuhudhuria maadhimisho ya Jamhuri Dei...

Jamhuri 2023: Mudavadi akaribisha wageni Ikulu ya Rais...

T L