• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 5:55 AM
Spika Kingi asalimu amri ya mahakama na kumruhusu Seneta Orwoba kurejelea shughuli zake za kawaida katika Seneti

Spika Kingi asalimu amri ya mahakama na kumruhusu Seneta Orwoba kurejelea shughuli zake za kawaida katika Seneti

NA CHARLES WASONGA

SENETA Maalum Gloria Orwoba sasa anaweza kuendelea kuhudhuria vikao vya Seneti, Kamati zake pamoja na kushiriki shughuli nyingine zote za bunge hilo.

Hii ni baada ya Spika wa bunge hilo, Amason Kingi kubatilisha hatua ya kumzima seneta huyo kwa miezi sita kwa mienendo mibaya.

Katika uamuzi aliotoa Jumanne, Oktoba 17, 2023, spika Kingi alisema kuwa bunge hilo litatii agizo la mahakama kwamba hatua hiyo ibatilishwe.

Hata hivyo, alieleza kusikitishwa na hatua ya Mahakama Kuu ya kumpa afueni Bi Orwoba aliyesimamishwa, kwa muda, kutia guu katika seneti kwa kutoa madai ya kuwakosea heshima maseneta wenzake na Karani wa Seneti Jeremiah Nyegenye.

“Tunalinda haki yetu ya kutetea hatua yetu kortini kuonyesha kuwa Seneti ilimpa Seneta nafasi ya kujitetea kwa njia ya haki,” spika Kingi akasema.

Seneta Orwaba, ambaye amekuwa akizingirwa na utata, alisimamishwa kuhudhuria shughuli za Seneti kwa miezi sita mnamo Septemba 20, 2023. Uamuzi huo uliafikiwa na Kamati ya Seneti kuhusu Mamlaka na Hadhi inayoongozwa na spika Kingi.

Alipewa adhabu hiyo baada ya kutoa madai kwamba baadhi ya maseneta wa kiume na Bw Nyegenye walipania kumnyanyasa kimapenzi.

Baadaye adhabu hiyo iliidhinishwa kwenye kikao cha Bunge lote. Hii ilimaanisha kuwa Seneta Orwoba hangeshiriki shughuli za Seneti hadi Februari 2024.

Aidha, angezuiwa kupokea manufaa yote na marupurupu isipokuwa mshahara wake wa kila mwezi pekee.

Lakini mnamo Oktoba 12, 2023, Mahakama ya Machakos ilibatilisha kwa muda adhabu hiyo.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa maagizo zaidi kuhusu kesi hiyo mnamo Oktoba 25, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Wenye nyumba za kupanga wamulikwa kwa kukatalia...

Rapudo athibitisha kutengana na Amber Ray akilaumu...

T L