• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 9:17 PM
Aachiliwa kwa dhamana katika kesi ya ulaghai wa shamba

Aachiliwa kwa dhamana katika kesi ya ulaghai wa shamba

Na RICHARD MUNGUTI

DIWANI wa zamani Wadi ya Kabartonjo Kaunti ya Baringo anayekabiliwa na shtaka la kumlaghai Bw Joshua Kulei shamba la ekari 224 Nairobi, ameachiliwa kwa dhamana ya pesa tasilimu Sh1 milioni.

Bi Elizabeth Sote Chesang aliachiliwa na hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina, baada ya polisi kuthibitisha kwa kipindi cha miezi 10 ambayo hakufika kortini kujibu mashtaka 2022 alikuwa anaugua.

“Polisi wamethibitisha kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali za Kapsabet, Kericho na Nakuru kwa muda wa miezi 10,” kiongozi wa mashtaka  Bw Anderson Gikunda alimweleza hakimu.

Bw Gikunda alisema hapingi mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana kwa vile polisi wamethibitisha allikuwa amelazwa hospitali kwa miezi 10, mwaka uliopita.

Sote alikabiliwa na shtaka la kughushi hati ya umiliki wa shamba la Kulei ya hektari 89.4 (ekari 224) katika eneo la Kitisuru.

Mahakama ilielezwa kwamba Sote alianza kugawa shamba hilo na kuanza kuliuza.

Mshtakiwa amekana alimlaghai Geofrey Kiptoo Kiprop Sh6.5 milioni akidai atamuuzia hektari moja ya shamba hilo.

Hakimu alimwachilia Sote kwa dhamana na kumwamuru afike kortini Aprili 20, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti yatoa tahadhari watoto wengi wakiugua Rotavirus

Mshukiwa adai marehemu Sh1m

T L