• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Eritrea yafungua mipaka yake kuruhusu wakimbizi wa machafuko nchini Sudan

Eritrea yafungua mipaka yake kuruhusu wakimbizi wa machafuko nchini Sudan

NA TESFA-ALEM TEKLE

ASMARA, ERITREA

RAIS wa Eritrea Isaias Afwerki ametangaza kuwa mipaka ya nchi yake imefunguliwa kuruhusu raia wa Sudan na wale wa mataifa mengine wanaotoroka vita Sudan kuingia nchini humo.

“Eritrea imefungua mipaka yake na itaendelea kuwapokea raia wake na wale wa Sudana pamoja na raia wa mataifa mengine waliathirika na vita nchini Sudan. Itawapa msaada wowote wa kibinadamu kadri ya uwezo wake,” akasema Rais Isaias.

Kiongozi huyo alitoa tangazo hilo kwenye mahojiano yaliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga ya kitaifa ya Eritrea Jumatatu usiku.

Aidha, aliongea kwa Kiarabu kusisitiza kujitolea kwa Eritrea kusimama na raia wa Sudan huku akitoa ujumbe wa heri njema kwa watu wa Sudan. Alisema Sudan ilitoa hifadhi kwa raia wa Eritrea wakati wa vita vya ukombozi vilivyodumu miongo kadha.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Uchumi: Mahasla walemewa

Mtoto niliyempata anakuja na bahati ya ushindi –...

T L