• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Jeshi la Somalia laangamiza magaidi 100 wa Al-Shabaab

Jeshi la Somalia laangamiza magaidi 100 wa Al-Shabaab

NA MASHIRIKA

MOGADISHU, SOMALIA

JESHI la Kitaifa la Somalia (SNA) linaloungwa mkono na wanamgambo wa eneo hilo wanaoitwa Ma’awisley limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa Al-Shabaab.

Mbali na hayo, wanajeshi wake walikomboa zaidi ya vijiji 20 wakati wa operesheni za usalama zilizofanywa katika majimbo mawili ya kikanda siku ya Jumapili, serikali ilisema.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Utalii ilisema shughuli hizo ziliendeshwa katika majimbo ya Galmudug, Hirshabelle na Kusini-Magharibi.

“Kundi la kigaidi limekuwa likitumia miji hii kama ngome za kupanga mashambulizi yao ya kigaidi kwa vilipuzi na walipuaji wa kujitoa mhanga katika maeneo tofauti ya Somalia,” wizara hiyo ilisema katika taarifa iliyotolewa mnamo Jumapili jioni katika mji mkuu wa Mogadishu.

Ilisema wanamgambo hao wamesababisha ukatili kwa raia wa eneo hilo ambao wamewateka nyara na kuwaua, na mali zao kuharibiwa.

Serikali ilieleza dhamira yake ya kuliondoa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab, ambalo ni tishio kwa watu wa Somalia, kutoka katika ngome zake.

“Kundi la kigaidi kwa zaidi ya muongo mmoja limefanya ukatili dhidi ya raia katika mji ambao wameudhibiti,” wizara hiyo ilisema.

Kundi hilo ambalo linapigania kupindua serikali limekuwa likikabiliwa na shinikizo kubwa na mashambulizi kutoka kwa vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na wanamgambo wa eneo hilo ambao wanataka kuwaondoa kutoka eneo la Hiran katikati mwa Somalia.

Al-Shabaab walifukuzwa Mogadishu mwaka 2011 lakini kundi hilo la kigaidi bado lina uwezo wa kufanya mashambulizi katika majengo ya serikali, hoteli na maeneo yaliyo na watu wengi.

Mapema Septemba mwaka huu, Wapiganaji wa Al-Shabaab waliwaua takriban raia 19 na kuharibu malori yaliyokuwa yamebeba chakula cha msaada katika shambulio la usiku katika eneo la kati la Somalia.

Kundi hilo lililojihami lilianzisha mashambulizi katika eneo la Hiran katika jimbo la Hirshabelle katikati mwa Somalia.
Malori hayo yalikuwa yakisafirisha chakula kutoka mji wa Baladweyne hadi mji Mahas kwa mujibu wa wenyeji.

“Magaidi hao waliwaua raia wasio na hatia waliokuwa wakisafiri … jana usiku. Hatuna idadi kamili ya wahasiriwa, lakini maiti 19 zimekusanywa,” mzee wa ukoo Abdulahi Hared aliambia shirika moja la habari.

“Maiti bado zinakusanywa, wakiwemo wanawake na watoto. Miili yao huenda ikawa zaidi ya 20,” alisema Bw Ali Jeyte, gavana wa eneo la Hiran ambako shambulio hilo lilitokea.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Ruto ataanza utawala wake vibaya iwapo...

Mfalme Charles III aahidi kufuata nyayo za mamake

T L