• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 8:55 AM
Kaburi la waliofariki bahari ya Shamu lazinduliwa Tunisia

Kaburi la waliofariki bahari ya Shamu lazinduliwa Tunisia

Na AFP

WAHAMIAJI wanaofariki katika bahari ya Shamu wakijaribu kuhamia bara Ulaya, sasa watakuwa na pahala pa kupumzishwa salama nchini Tunisia.

Hii ni baada ya serikali ya Tunisia kuzindua rasmi makaburi ya kuwazika watu hao ambayo tayari nusu ya nafasi yake ishatumiwa kwa shughuli hiyo.Mkuu wa kitengo cha utamaduni wa Shirika la Umoja wa Kimataifa la UNESCO, Audrey Azoulay, akizungumza wakati wa hafla hiyo, alisema hilo litasaidia kuwapa wanaofariki mazishi ya heshima.

Wengi waliozikwa katika makaburi hayo ni wahamiaji ambao majina yao hayafahamiki wala hayajaandikwa walikozikwa. Hata hivyo, makaburi hayo yamezingirwa na mandhari mazuri kupitia upanzi wa maua na miti.Msanifishaji mijengo kutoka Algeria ambaye alifadhili na kuchora ramani ya makaburi hayo, alisema alilenga kuhakikisha marehemu hao wanapewa pumziko zuri la amani.

 “Hii ni ya kuwapa wanafamilia wa wapendwa hao amani na kufahamu kuwa wenzao waliopatikana na maafa wakiwa na nia ya kusaka maisha mazuri wamepewa mazishi ya hadhi,” akasema mmoja wa waliohusika na mpango huo, Rachid Koroichi.

Na AFP

  • Tags

You can share this post!

Agizo la Magoha kuhusu karo linakiuka ahadi ya serikali

ICC yataka mibabe sita wa vita Sudan wasalimishwe