• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Marufuku ya minisketi UG hatimaye yafutwa

Marufuku ya minisketi UG hatimaye yafutwa

Na Mashirika

MAHAKAMA imefutilia mbali sheria iliyopiga marufuku wanawake kuvaa nguo fupi, almaarufu minisketi baada ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati.

Sheria ya kupiga marufuku usambazaji wa picha za ngono ilipitishwa 2014 na walioiunga mkono walisema kuwa ilinuia kuwalinda wanawake na watoto.

Lakini wakosoaji wake wanasema kuwa sheria hiyo ilitumiwa vibaya na kusababisha baadhi ya wanawake na wasichana walioonekana wamevalia mavazi mafupi kushambuliwa mitaani.

Sheria hiyo ilifutiliwa mbali na jopo la majaji watano wa Mahakama ya Katiba ya Uganda.Majaji hao walikubaliana kwa kauli moja kwamba vifungu vya sheria hivyo vilivyoharamisha ‘mavazi yanayoonyesha uchi’, vinakiuka Katiba.

Walisema kuwa hakutakuwa na madhara yoyote kwa wanawake na wasichana kuvaa nguo wanazozipenda.Kupitishwa kwa sheria hiyo – iliyopewa jina la sheria ya minisketi – kulisababisha maandamano jijini Kampala baada ya wanawake waliopatikana na nguo fupi kudhulumiwa mitaani.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu waliitaka serikali kufutilia mbali sheria hiyo na baadaye walienda mahakamani kuipinga.

 

You can share this post!

Agizo Shirika la Huduma za Feri lifidie kampuni Sh5.2...

Rais aongoza Wakenya kuomboleza seneta aliyefariki kwa ajali