• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Agizo Shirika la Huduma za Feri lifidie kampuni Sh5.2 milioni

Agizo Shirika la Huduma za Feri lifidie kampuni Sh5.2 milioni

Na Philip Muyanga

SHIRIKA la Huduma za Feri nchini (KFS) limo hatarini kupoteza baadhi ya mali zake kwa mnada baada ya kushindwa kusitisha agizo la mahakama linalohitaji kampuni ilipwe Sh5.2 milioni.

KFS ilikuwa imeagizwa kulipa pesa hizo kwa kampuni ambayo lori lake lilitumbukia baharini lilipokuwa likiabiri feri katika kivuko cha Likoni, Kaunti ya Mombasa.

Jaji Eric Ogola alitupilia mbali ombi la KFS na kusema shirika hilo halikutoa sababu za kuridhisha kutaka agizo hilo libatilishwe.

Jaji alisema KFS ililalamika kuwa haikupewa stakabadhi za kesi, lakini kampuni ya Madale Tracking Co iliwasilisha ushahidi kutimiza hayo.

Kampuni hiyo ilishtaki KFS mwaka wa 2014, wakati ambapo shirika hilo la feri lilikuwa na bima kutoka kampuni ya African Merchant Assurance Company Ltd (Amaco).

Kampuni hiyo ilikuwa imekubali kulipwa fidia kwa mgai wa kila mwezi, lakini KFS iliposhindwa, mahakama ikatoa uamuzi Mei 12, 2020 na kuruhusu kampuni hiyo kupiga mnada mali za KFS.

Shirika hilo limelalamika kuwa, agizo hilo litafanya kuwe na lalama kuhusu utumizi mbaya wa fedha kwani hakuna bajeti ya kugharamia kiwango hicho cha fedha kinachotakikana.

You can share this post!

Ghost Mulee kupigwa jeki na kuwasili kwa Olunga

Marufuku ya minisketi UG hatimaye yafutwa