• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:55 AM
Raila alalamikia Kenya Kwanza kuendelea ‘kununua’ wabunge

Raila alalamikia Kenya Kwanza kuendelea ‘kununua’ wabunge

Na SAMMY WAWERU

KINARA wa Azimio la Umoja Raila Odinga ameisuta kwa mara nyingine serikali ya Kenya Kwanza akidai ina njama kuzima upinzani nchini.

Akirejelea suala la baadhi ya wabunge wa muungano wa Azimio waliojiunga na serikali, Bw Odinga alisema taratibu zilizotumika hazikufuata sheria.

“Kenya Kwanza inaendelea kununua wabunge bila kufuata sheria. Sheria imewekwa wazi, mbunge anapojiunga na mrengo mwingine anapaswa kujiuzulu na kutafuta upya wadhifa anaoshikilia,” alisema.

Baadhi ya wabunge waliochaguliwa Agosti 9, 2023 wametekwa na serikali ya Kenya Kwanza, inayoongozwa na Rais William Ruto.

“Hatujaona hilo likifanyika (kujiuzulu na kurejea debeni kupitia muungano ambao mwanasiasa amejiunga nao),” akasema Raila Odinga.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alitoa malalamishi hayo wakati akihutubia wanahabari jijini Nairobi, ambapo anapinga Mswada wa Fedha 2023 unaopendekeza nyongeza ya ushuru (VAT) kwa bidhaa kama vile petroli, mishahara (kugharamia ujenzi wa makazi ya bei nafuu) na biashara zinazoendelezwa kidijitali.

Endapo mswada huo utapitishwa na bunge, VAT ya mafuta ya petroli itaongezeka kutoka asilimia 8 hadi 16.

Nyongeza hiyo itaashiria mzigo mzito kwa mlipa ushuru, hususan wananchi wa mapato ya chini ikizingatiwa kuwa gharama ya maisha ni ghali.

  • Tags

You can share this post!

Wadudu hatari aina ya Mbung’o wangali tishio kwa...

Gachagua: Machifu 20 na manaibu kufutwa kwa kushindwa...

T L