• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Wadudu hatari aina ya Mbung’o wangali tishio kwa mifugo

Wadudu hatari aina ya Mbung’o wangali tishio kwa mifugo

Na GEORGE ODIWUOR

UVAMIZI wa mbung’o bado ni tishio kuu kwa wakulima wengi wanaoshiriki ufugaji katika Kaunti ya Homa Bay.

Wadudu hao husababisha maradhi yanayofahamika kama nagana kwa mifugo na malale kwa binadamu.

Wanyama wanapoumwa na wadudu hao, ngozi yao huharibika na hata kusababisha maafa.

Baraza la Kuangamiza mbung’o na Malale Kenya (Kentec) linasema kuwa mifugo kadhaa wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika maeneo tofauti kwenye bonde la Lambwe lenye kiwango cha juu zaidi cha maradhi hayo na wadudu hao.

Msimamizi wa Kentec katika maeneo ya ziwani, Bernard Chemweno, alisema kiwango cha maambukizi ya maradhi hayo kinatofautiana kutegemea na hali ya anga.

“Wadudu hao huongezeka kwa kasi katika msimu wa mvua ikilinganishwa na msimu wa kiangazi. Kiwango cha maambukizi ya gonjwa hilo hubadilika kati ya asilimia 3 na 13 kutegemea hali ya anga,” alisema.

Juhudi za hapo awali za kudhibiti wadudu hao na kuangamiza ugonjwa huo zimefanikiwa katika maeneobunge ya Suba Kaskazini.

Dalili za gonjwa hilo bado zinapatikana katika baadhi ya vijiji vinavyozingira Mbuga ya Kitaifa ya Wanyamapori ya Ruma inayosheheni wadudu hao kwa wingi.

Mbunge wa Suba Kusini, Caroli Omondi, aliwasilisha pendekezo akiitaka serikali ya kitaifa kubuni mfumo mpya kuwasaidia wakulima wanaoadhirika na maradhi hayo.

Amependekeza wahasiriwa kufidiwa kufuatia vifo vya Wanyama wao kutokana na kuumwa na wadudu hao.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge Homa Bay waingia boksi ya Gavana Wanga

Raila alalamikia Kenya Kwanza kuendelea ‘kununua’...

T L