• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Wasiwasi Ghana wabunge 15 wakiugua corona

Wasiwasi Ghana wabunge 15 wakiugua corona

Na AFP

Bunge la Ghana litakuwa likifanya vikao vyake mara mbili kila wiki, spika wa bunge hilo amesema.

Bw Alban Bagbin ametoa tangazo hilo baada ya wabunge 15 na wafanyakazi kadhaa kupatikana wameambukizwa virusi vya corona.

“Kati ya waliojitokeza bungeni kufanyiwa ukaguzi na vipimo, wabunge 15 wamepatikana na Covid-19 na wamearifiwa kuhusu hali yao na kushauriwa wajitenge,” akasema.

Spika huyo pia amefichua kwamba wafanyakazi 56 wa bunge wamethibitishwa kuambukizwa corona, hali ambayo imemlazimisha kupunguza vikao vya bunge kuwa siku ya Jumanne na Alhamisi pekee kila juma.

Bw Bagbin alisema hatua hiyo itasaidia kuzuia kuenea kwa Covid-19 bungeni.

Tangazo la spika huyo limejiri siku chache baada ya Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo mnamo Jumapili kurejesha marufuku ya mkusanyiko wa umma na ummati kufuatia kuendelea kuongezeka kwa visa vya wagonjwa wa corona nchini humo.

Shule Ghana zilifunguliwa Januari 2021, miezi kumi baada ya kusalia kufungwa, taifa hilo lilipothibitisha kuwa mwenyeji wa ugonjwa wa Covid-19 na ambao ni janga la kimataifa.

Rais Akufo-Addo mnamo Jumapili aliashiria kukaza kamba sheria na mikakati kudhibiti maambukizi zaidi kufuatia ongezeko la visa vya wagonjwa.

Kwa sasa, Ghana inaandikisha wastani wa maambukizi mapya 700 kila siku, kutoka takwimu za awali, wagonjwa 200.

Tafsiri: SAMMY WAWERU

  • Tags

You can share this post!

Django FC inavyokuza talanta za chipukizi wa Uthiru

Ighalo apata hifadhi Saudia