• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Carrol Sonie, Mulamwah waambiwa watoto si wa kuingizwa kwa mzozo wao

Carrol Sonie, Mulamwah waambiwa watoto si wa kuingizwa kwa mzozo wao

NA FRIDAH OKACHI

MWIGIZAJI Caroline Muthoni almaarufu Carrol Sonie amechukua hatua ambayo baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanahisi ni uamuzi wa haraka mno aliofanya baada ya Ruth K kuthibitisha amebeba mimba kutokana na uhusiano wake na David Oyando almaarufu ‘Mulamwah’ ambaye ni ex wake. 

Katika kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa mashabiki wake kwenye mtandao wa YouTube, Sonie alisema alishaliondoa jina la Mulamwah kwenye cheti cha kuzaliwa cha mwanawe na kutaja majina yote mapya kuthibitisha kwamba ex wake huyo hana lolote katika maisha ya binti yake.

“Majina ya binti yangu yote si ya Kingereza… Ahsante sana kwa swali hilo,” Sonie alisema na kulitaja jina jipya la mwanawe.

Lakini baadhi ya mashabiki na wakosoaji wake wamedai kuwa hatua hiyo ni sawa na kujaribu kuzima mizizi ya ukoo wa mwanawe.

Diana Mwangangi alikerwa na hatua hiyo na kunukuu sheria ya watoto ya mwaka 2022 akisema wazazi wote wana haki.

“Hakuna mzazi mmoja aliye na uhuru wa kumtunza mtoto peke yake isipokuwa kama kuna ushahidi wa unyanyasaji kutoka kwa mzazi mwenzake. Watu wanahitaji kufahamu sheria vyema na kila mara waangalie athari zinazoweza kusababishwa na matendo yao kwa maisha ya baadaye ya watoto wao. Tafadhali ondoa watoto kwenye migogoro ya mahusiano yako. (Watoto) si silaha za kupigana, mtawaumiza!” alichangia Bi Mwangangi.

Pia, Sonie aliulizwa swali mmoja kuhusu changamoto kuu ambayo amekuwa akipitia katika malezi ya bintiye ambapo alisisitiza kwamba hajawahi kushirikiana katika malezi na Mulamwah, akisema ni wazazi wake ambao humsaidia kumlea mtoto huyo.

Mwigizaji huyo alienda hatua zaidi kudai kwamba hali anayopitia inahitaji mwanamke kujipa moyo na kusonga mbele.

Haya yanajiri wiki chache baada ya Ruth K kufichua ni mjamzito.

  • Tags

You can share this post!

Beki Dorcas Shikobe roho juu Stars wakielekea Gaborone kwa...

Wakazi wa Juja waisuta serikali kwa utepetevu fisi...

T L