• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Kang’ata awapa wenyeji Murang’a fursa ya ‘full kujiachia’

Kang’ata awapa wenyeji Murang’a fursa ya ‘full kujiachia’

NA MWANGI MUIRURI

GAVANA wa Murang’a Irungu Kang’ata mnamo Desemba 23, 2023, ataongoza wenyeji kupisha Krismasi katika densi itakayoandaliwa katika pahala patakatifu kimila kwa jamii ya Agikuyu, Mukurwe wa Nyagathanga.

Kwa wanaoamini itikadi za kale, wazazi wa jamii ya Agikuyu–Bw Gikuyu na Bi Mumbi–walikuwa wakiishi katika himaya hiyo ya Mukurwe wa Nyagathanga.

Inasemwa kwamba wawili hao walizaa mabinti 10 kwa majina Wanjiru, Wambui na Wanjiku. Wengine walikuwa Wangui pia akifahamika kama Waithiegeni, Wangeci au Waithira, Wanjeeri au Waceera, Nyambura au Wakiuru, Wairimu au Gathiigia, na Wangari na ambao waliishia kuunda koo tisa za jamii hiyo kupitia ndoa kwa wanaume ambao haijafafanunuliwa vyema walitoka wapi ikizingatiwa hakukuwa na familia nyingine isipokuwa hiyo ya Gikuyu na bibi yake Mumbi.

Hata hivyo, Wamuyu ambaye alikuwa binti wa 10 kwa wawili hao, inasemekana hakuolewa.

Katika densi hiyo, waimbaji wa nyimbo za ushauri na pia za Injili kutoka jamii hiyo watatumbuiza watakaofika hapo kujiachia.

Wasanii hao ni pamoja na Ben Githae, Samidoh, Kariuki wa Kiarutara, Joyce wa Mamaa, Kamoko, Gathee wa Njeri ambaye pia ni diwani wa Gaturi, Phyllis Mbuthia, Ngaruiya Junior, Loise Kim, na Kuruga wa Wanjiku.

Aidha, makundi ya nyimbo za kiasili kutoka eneo hilo watatumbuiza wageni.

Gavana Kang’ata katika taarifa rasmi kuhusu hafla hiyo alisema densi hiyo pia itatumika kuwakumbuka mashujaa wa ngoma wa kaunti hiyo walioaga dunia kama John De Mathew, Queen Jane, George Wanjaro, na Joseph Kamaru.

Bw Kang’ata alisema kwamba hakuna ada itatozwa wenyeji kufika katika densi hiyo ya kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni na ambayo kuanzia saa nane, itapeperushwa moja kwa moja na baadhi ya vituo vya runinga vinavyotangaza kwa lugha ya Gikuyu.

  • Tags

You can share this post!

Kamanda wa kituo cha polisi Vihiga ajeruhiwa kwa kisu na...

Balala afikishwa mahakamani Malindi kwa kesi ya ufujaji...

T L