• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Nakubali tatizo ni mimi, Akothee asema akirejelea mahusiano yake yasiyodumu

Nakubali tatizo ni mimi, Akothee asema akirejelea mahusiano yake yasiyodumu

NA SINDA MATIKO

AKOTHEE anadai kuwa kujipenda kwake kupita maelezo ndio kumemkosti ndoa zake. Baada ya ndoa yake ya pili kudumu kwa miezi miwili tu, huku pia mahusiano yake kadhaa yakinyauka, Akothee kaishia kuamini kuwa yeye ndio chanzo.

Mama huyo wa wana watano sasa anasema kwamba, amegundua hakuumbiwa mahusiano na ndio maana yamekuwa yakifeli.

“Mimi ni mwanamke ninayejipenda sana tena kupita maelezo. Huwa nahisi najipenda kupitiliza kiasi kwamba inakuwa mzigo kwa mtu ambaye nipo kwenye mahusiano naye, na ndio sababu mimi ni Afisa Mkuu wa ndoa zilizofeli. Kwa namna ninavyojipenda mimi, mtu akinizengua kidogo tu, huyo mimi nakanyaga kubwa kubwa. Mahusiano sikuumbiwa mimi ila kama ni kwenye biashara, basi mimi ni mwalimu,” anasema.

Mapema mwaka huu Akothee alifunga ndoa yake ya pili na mzungu Denis Schweizer almaarufu Omosh lakini haikudumu zaidi ya miezi miwili.

***

Rufftone awalima vijembe

MWANAMUZIKI mkongwe wa injili Rufftone, kawalima vijembe wasanii wote walioiacha tasnia ya injili kufanya muziki wa kidunia.

Wengi wa wasanii hao waliovuka boda, walidai kufanya hivyo ili kusaka mpunga zaidi. Miongoni mwao wapo Kevin Bahati, Willy Paul kati ya wengine.

Sasa Rufftone anahoji ni kwa nini wasanii wote hao walioiacha tasnia ya muziki wa injili hawatambi huko kwenye muziki wa kidunia.

“Nionyeshe msanii mmoja aliyeiacha tasnia ya injili ambaye kwa sasa anatamba kwenye tasnia ya muziki wa kidunia. Yeye ndio anapata shoo nyingi, yeye ndiye ngoma zake zinapigwa sana yani ni yeye ndio yupo kwenye chati. Nitajie hata mmoja. Hawapo,” Rufftone anasema.

Kulingana naye, wasanii wengi walioiacha injili toka mwanzoni hawakuwa na nia ya kufanya muziki wa injili ila walikuwa wakisaka fursa tu rahisi ya kujisukuma kwenye chati.

***

Mtalipwa, Clemmo ahakikishia wasanii waliotumbuiza Nairobi Festival

PRODUSA mkongwe wa muziki Clemmo ambaye kwa sasa ni waziri wa Sanaa katika Kaunti ya Nairobi, amewafutia hofu ya malipo wasanii wote watakaotumbuiza kwenye tamasha ya Nairobi Festival.

Tamasha hiyo ya siku sita ilianza kwenye sherehe za Jamhuri Dei ikiwa ni makala ya pili.

Baada ya makala ya kwanza ya mwaka jana wakati kama huu, miezi miwili baadaye, mwanamuziki Arrowbowy, aliibuka na kutangaza kuwa bado hajapokea malipo yake.

“Wakenya hunifurahisha sana, mbona baada ya kulipwa waliokuwa wakilalama hawakujitokeza kutangaza hilo pia. Watu waelewe kuwa hela hizi tunazotumia ni za umma na kuna utaratibu wa kuzitoa sio kama hii ni biashara binafsi jinsi inavyokuwa kwenye tamasha zingine. Kwa sababu hiyo wakati mwingine utaratibu huchukua muda kidogo. Kwa maana hiyo hata kwa makala ya mwaka huu, watu wawe na subira ikifikia suala la malipo watapokea hela yao,” amekata kauli Clemmo

  • Tags

You can share this post!

Mtaalamu: Ugumu wa maisha unavyoathiri ukuaji wa watoto...

Afueni kidogo, bei ya mafuta ikishuka Desemba

T L