• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
DINI: Utavuna ulichopanda, hakuna mkato maishani!

DINI: Utavuna ulichopanda, hakuna mkato maishani!

NA WYCLIFFE OTIENO

WAKATI mwingi tunapoona mafanikio ya watu wengine, tunatamani kuwa kama wao.

Tunatamani kuitanishwa nao. Kile tusichokitilia maanani ni kuwa kuna gharama waliyoilipa kufikia pale.

Mambo hayaji tu kirahisi.

Wachezaji wazuri, wanapanda mbegu ya mazoezi kwa bidii.

Wanafunzi wazuri wanapanda mbegu ya kusoma kwa bidii. Kurudiarudia ni mama wa kusoma, alisema Andrew Jackson.

Wafanyikazi wanaoheshimika wanapanda mbegu ya bidii, wanamakinika na wanatii maagizo ya viongozi wao.

Kunyenyekea ni mbegu ya mtu anayetaka kuinuliwa.

Kusikiliza kwa makini ni mbegu ya mtu atakaye kujifunza. Kusamehe ni mbegu ya mahusiano ya kudumu. Kuomba kwa bidii na kufunga, kusoma neno na kuwa katika ushirika na wengine ni mbegu ya anayetaka kuwa kiroho.

Kuna mbegu unayohitaji kupanda ili upate unachotarajia. Wagalatia 6:7-9 yasema, Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

Kwa kiwango unachopanda utavuna. Kuna watu wakitenda jambo jema mara moja wanatarajia makubwa milele.

2 Wakorintho 9:6 yasema, Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

Ibrahimu alikaribisha malaika. Alipanda ukarimu. Ahadi iliyokuwa haina tarehe ikapewa tarehe.

Mwanzo 18:10, Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume.

Dorkasi alipokufa, wajane walikumbuka matendo yake ya ukarimu jinsi alivyowashonea mavazi. Walimsihi Petro amwombee. Hatimaye alifufuka.

Matendo yako mazuri yatakumbukwa ukiwa kwenye tatizo na ukombozi utapatikana

Hata watu wanaoonekana kuwa wabaya, matendo yao mema hukumbukwa.

Yoshua alimhifadhi Rahabu, na watu wa nyumba ya baba yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko.

Lakini pia hekima yahitajika kuhusu mahali panapofaa. Kuna mtu alipenda dagaa sana. Kwa kuwa alikuwa mtu wa bara, alidhani wanatoka shambani. Alipanda kilo kumi shambani mwake. Hawakumea.

  • Tags

You can share this post!

Shujaa wazidiwa maarifa Hamilton 7s kujiweka pabaya zaidi...

FATAKI: Ajabu kuu ‘wife material’ kuwa mwanamke...

T L