• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
DKT FLO: Dawa kupunguza uzani upesi gani?

DKT FLO: Dawa kupunguza uzani upesi gani?

Mpendwa Daktari,

Kwa miezi kadhaa sasa nimeshuhudia uzani wangu ukiongezeka. Kuna dawa hususan ya kupunguza uzani upesi?

Christine, Nairobi

Mpendwa Christine,

Tatizo la uzani mzito mara nyingi huwa ni kutokana na kupungua kwa kasi ya umetaboli mwilini, hali ambayo huanza katika miaka ya 20 na 30.

Wakati mwingi uzani huongezeka zaidi bila ya sisi kugundua mwanzoni na hatimaye kuwa tatizo.

Hali huwa mbaya zaidi hasa kutokana na mabadiliko ya viwango vya homoni, kutozingatia lishe bora na kutofanya mazoezi ya kutosha.

Hii inamaanisha kwamba unahitaji kiwango cha chini cha chakula na hivyo nishati kidogo ili mwili kuendesha shughuli zake.

Mbinu bora ya kukabiliana na uzani wa ziada ni kupunguza kiwango cha kalori na kuongeza shughuli za mazoezi kwa kipindi kirefu.

Kwa hivyo unapaswa kuchagua lishe bora, vilevile kuwa na ratiba ya mazoezi yanayokufaa.

Aidha, waweza pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe, na pia mkufunzi wa mazoezi.

Japo ni kawaida kukumbwa na majaribu ya kutaka kupunguza uzani kwa kasi, ukweli ni kwamba mara nyingi mbinu zisizo za kiafya haziwezi dumishwa kwa muda mrefu.

Hii ni kwa sababu dawa nyingi za kupunguza uzani zina madhara kama vile tumbo kuvimba, mwili kutetemeka na hata mhusika kutawaliwa nazo.

You can share this post!

Karamu ya mbuzi yaokoa mshukiwa wa mauaji

Wawili washtakiwa kuteka nyara polisi

T L