• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Kanisa la ACK Kajiado linavyohamasisha wakazi jinsi ya kuangazia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa  

Kanisa la ACK Kajiado linavyohamasisha wakazi jinsi ya kuangazia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa  

NA FRIDAH OKACHI

KANISA la ACK eneo la Elapolos, Kajiado Kaskazini, limetoa mafunzo za dhuluma ya kijinsia, namna wakazi wanavyoweza kuripoti katika vituo vya polisi licha ya mazungumzo ya kanisa kufeli.

Mmoja wa kiongozi wa kanisa hilo Loice Baya amesema wamekuwa wakipokea visa hivyo kuripotiwa katika kanisa hilo, wengi wao wakikosa kufahamu jinsi ya kuripoti.

Bi Baya aliambia Taifa Leo Dijitali, juma liliopita, katika mtaa wa Embubul kumekuwa na visa vya kutamausha baada ya kupokea visa viwili vya wanaume wawili kuwakatakata wake zao baada ya kutofautiana.

“Ukiona mambo yamezidi, usingoje kukatwa katwa ufe, si mnajua vile mambo yalifanyika katika mtaa huu, msinyamazie hali hiyo. Vituo vya polisi vina vitengo vya kuripoti unapodhulumiwa na mke au mume, na kama kanisa tutawaleta pamoja tuwasikize mkirudi nyumbani mnazozana tena,” Bi Baya akambia waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.

Loice Baya akizungumza na wanawake na wanaume katika kanisa la ACK, Kajiado Kaskazini kuhusu dhuluma za jinsia. PICHA| FRIDAH OKACHI

“Tumetoa mafunzo hayo kuhakikisha tunaangazia dhuluma hizi ambazo zimezidi. Jamii hapa inadhulumiwa kwa njia moja au nyingine lakini hawajui mahali ambapo wanapaswa kuripoti,” Bi Baya alisema.

Wanawake na wanaume waliokuwa walihamasishwa kuripoti visa hivyo katika vituo vya polisi ili kupata usaidizi.

Jane Naseya ambaye ni mwalimu, alisema kufahamu utaratibu atakaotumia kuripoti visa vya dhuluma utamfaa pakubwa katika kuangazia dhuluma za kijinsia.

“Mimi ni mwalimu, na kupitia mafunzo hayo nimefahamu jinsi jamii yangu inanyanyaswa na hatua mahususi kuchukua visa vinapoibuka. Mimi kama mke, nimeshauriwa sio kila dhuluma nahitaji kunyamazia kwenye ndoa. Ni vizuri nipige ripoti nipate usaidizi,” Bi Naseya akasema.

Utafiti wa Kenya Demographic and Health, unaonyesha wanaoathirika na dhuluma ni wanawake na wanaume walio kati ya miaka 15 hadi 49, Kaunti ya Kajiado ikiandikisha asilimia 38 ya visa vya dhuluma.

  • Tags

You can share this post!

Gavana Nassir ataka kujua ziliko pesa za El-Nino

Huzuni mtoto Homa Bay akifariki kwa kutumbukia kwenye uji...

T L