• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 11:59 AM
Ploti ya Onyesho la Kwanza tendo la tatu katika tamthilia ‘Kigogo’

Ploti ya Onyesho la Kwanza tendo la tatu katika tamthilia ‘Kigogo’

Na SIMON NGIGE

JUMA lililopita tulianza kuangalia ploti katika onyesho la kwanza tendo la tatu.

Majoka anahema. (mtindo-taswira) Anajaribu tena kumpa Ashua maneno matamu na kuusifia urembo wake usio na mfano. (maudhui-mapenzi, uk. 20)

Ashua anapomwita Mzee, Majoka anakasirika sana na kumwonya vikali. Anamwambia Ashua kuwa subira yake imeanza kufunganya virago. (mtindo – tashhisi). Anaona kuitwa Mzee ni kukosewa heshima. Kwa unyenyekevu Ashua anamwomba radhi. (toni ya unyenyekevu), (sifa ya Ashua-mnyenyekevu, maudhui-unyenyekevu). Ashua anaposema samahani Ngao. Majoka anafurahia sana jina hilo linapotajwa na kupiga makofi ya furaha. Ni jina lake la ujanani. Anamjongea tena Ashua anayeonekana kuhofia jambo. (mtindo-taharuki). ‘Njoo mahabuba, nikupe huba’ (mtindo urudiaji wa silabi ba)

Anajaribu tena kumbusu lakini Ashua anaruka kando na kumwambia Majoka hawezi kumkumbatia. (maudhui-uaminifu katika ndoa). Majoka anasema talaka kwa Ashua ni baraka kwake Majoka. Ashua anasema amekuja kuomba msaada wa chakula kwa sababu kina Pili na Pendo wanalala njaa. Majoka anamkejeli kuwa anamfyoa kwa sababu hao watoto si wake Majoka. Ashua anaanza kudondokwa na machozi na kutaka kupiga magoti. Majoka anaona machozi ya mseto wa mapenzi na majuto (mtindo-tanakuzi). Anamshika Ashua mkono, anamnyanyua na kufaulu kumkumbatia. Anamwambia kwa sauti ya chini ya kumpembeja kuwa aseme na ampendaye na aache kulia badala yake astarehe kwenye kifua cha shujaa wake. (mtindo-taswira uk.22). Ashua kwa mnong’ono anasema kuwa wamelala njaa-hawajala baada ya soko kufungwa.

Majoka anamwambia kuwa asijali (uk. 23). Anamwambia haja zake Ashua ni za Majoka pia, na kiu ya Ashua pia ni ya Majoka-bora maelewano tu. (mtindo-kinaya, maudhui-uzinifu). Majoka anataka kumpiga busu. Ashua anajifurutua na kuruka kando karibu na mlango. Majoka anamwuliza anarukaje kama kiroboto? (mtindo-tashbihi).

Simon Ngige

Shule ya Upili ya Alliance

You can share this post!

NBC: Chama cha Uanahabari katika shule ya Upili ya Ndalani,...

KAULI YA PROF IRIBE: Kiswahili kingetaja maazimio haya 2022...

T L