• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Bajia za bizari nyembamba na sosi ya ukwaju

MAPISHI KIKWETU: Bajia za bizari nyembamba na sosi ya ukwaju

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 2

Vinavohitajika

  • Kitunguu maji 1 kilichokatwakatwa
  • Punje 4 za kitunguu saumu, menya
  • Mashina machache ya dania
  • Kikombe 1 cha ketchup
  • Vijiko 3 vya asali
  • Kikombe ¼ ubandiko wa ukwaju
  • Kijiko ½ poda ya giligilani
  • Kijiko ½  cha pilipili
  • Kijiko ¼ cha manjano
  • Kijiko ¾ cha bizari nyembamba
  • Kikombe 1 cha unga wa dengu
  • Maji
  • Viazi mbatata vilivyokatwa
  • Kijiko 1 cha majani ya rosemary

Maelekezo

Katika sufuria, ongeza mafuta kidogo na chumvi. Ongeza vitunguu maji ulivyokatakata, vitunguu saumu na mashina ya dania na upike hadi vilainike.

Ongeza pilipili na viungo vya poda ya giligilani; changanya, na kisha ongeza asali, uweke ukwaju na ketchup.

Changanya vyote na uruhusu vichemke kwenye moto mdogo hadi mchanganyiko uwe mzito.

Hii itachukua kama dakika 10-15. Onja na urekebishe kwa kiungo chochote ikihitajika. Na kumbuka, kama kiungo kingine chochote, ikiwa umezidisha ukwaju, utafanya mchuzi kuwa chachu sana.

Epua.

Kwa kuandaa bajia, kwenye bakuli kubwa, weka unga wa dengu pamoja na viungo kavu na chumvi pia.

Changanya viungo vya kavu ndani na kisha ongeza maji kidogo kidogo huku ukiendelea kuchanganya.

Mkorogo wako unapaswa kuwa mzito kama mtindi. Ikiwa ni mwepesi sana, utateleza kutoka kwa viazi vyako. Ikiwa ni mzito sana, utazuia bajia zako hivyo hazitaiva ndani.

Kisha ongezea rosemary na giligilani.

Weka viazi katika mchanganyiko wako na kisha kwenye mafuta yaliyo moto, kaanga juu ya joto la kati. Usiruhusu viazi kukaa kwa muda mrefu kwenye mafuta.

Bajia zikiiva, pakua na sosi ya ukwaju, asali, mboga mboga na kuku pia ukipenda.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi ya kuondoa chunusi

DOUGLAS MUTUA: Wahamiaji walivyogeuza mkondo wa siasa...

T L