• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa mukimo

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa mukimo

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MUKIMO ni chakula cha kiasili cha Wakenya na kimepata umaarufu sana miongoni mwa waishio mjini.

Pia ni chakula cha kawaida katika sherehe kama vile harusi, tamasha na karamu.

Mukimo hutengenezwa kwa viazi, njegere, mahindi na vitunguu.

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 35

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • kikombe 1 cha njegere
  • vikombe 2 vya mahindi
  • vitunguu maji 2
  • mafuta ya kupikia kikombe ΒΌ
  • viazi mviringo 20
  • chumvi
  • majani ya malenge

Maelekezo

Chambua viazi, vioshe vizuri kisha chemsha kwenye moto wa wastani kwa dakika 15. Baada ya hapo, viponde na uviweke kando.

Chemsha njegere na mahindi pamoja.

Chemsha kwa dakika tatu majani ya malenge ambayo utachanganya pamoja vingine ulivyoviandaa.

Kaanga vitunguu vyako – vya maji na saumu – katika sufuria tofauti kwenye moto wa wastani.

Vitunguu vikishakuwa na rangi ya kahawia, ongeza viazi ulivyochemsha awali. Ongeza mchanganyiko wa njegere zilizochemshwa na mahindi na uponde pamoja hadi umbile liwe laini.

Ongeza majani ya malenge yaliyochanganywa na chumvi kwa ladha.

Funika mchanganyiko na uache upikike kwa muda wa dakika mbili.

Chakula chako aina ya mukimo kiko tayari. Pakua kwenye sahani na ufurahie pamoja na kitoweo chako unachopenda.

You can share this post!

ODM, PAA watoana rangi katika kampeni kali Kilifi

BORESHA AFYA: Viazi mviringo

T L