• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 9:17 PM
MAPISHI KIKWETU: Mboga: Kuhifadhi ubora na utamu

MAPISHI KIKWETU: Mboga: Kuhifadhi ubora na utamu

Na PAULINE ONGAJI

MBOGA ni chakula muhimu kwa mwili na kukosa kula kiwango kinachohitajika huathiri kingamwili.

Lakini je, wajua kuwa kuna jinsi ambavyo unaweza zipika na kuathiri ubora wake?

Mbinu hizi zitakusaidia kuhifadhi ubora tokea kwa matayarisho, mapishi, hadi maandalizi:

•Suuza mboga zako vizuri kabla ya kuanza mapishi: Japo kusafisha mboga husaidia kukabiliana na uchafu, bakteria na wadudu, ukilowesha mboga zako kwa muda mrefu, basi utaharibu virutubisho muhimu kama vile vitamini C.

Ili kuhifadhi vitamini zinazoyeyuka majini, kata mboga zako kwa vipande vikubwa au hata ikiwezekana uzipike zikiwa nzima. Kwa mfano viazi vilivyookwa huhifadhi virutubisho vingi zaidi ya viazi vilivyopondwa.

Hakikisha unazingatia muda, halijoto na kiwango cha maji unayotumia wakati wa mapishi, ambapo unashauriwa kutumia kiasi kidogo cha maji. Hii ndio sababu mapishi kwa njia ya mvuke inaaminika kuwa bora zaidi unapopika chakula hiki.

•Zingatia mbinu ya mapishi: Mbali na kupika kwa mvuke, utafiti unaonyesha kuwa kutumia wimbi maikro huhifadhi asilimia 80 ya vitamini C. Kadhalika kuchoma baadhi ya mboga na kukaanga katika karai bapa pia ni mbinu nzuri.

Mboga za kukaangwa zinahitaji mafuta kidogo mradi unatumia mafuta ya uowevu. Kadhalika, ili kuimarisha ubora wake pia waweza ongeza kitunguu saumu ila usikiponde na badala yake ukate kwa vipande vikubwa ili uachilie vimeng’enya.

You can share this post!

MALEZI KIDIJITALI: Mbinu za kudhibiti vifaabebe

PSG watandika Brest na kufungua pengo la alama 11 kileleni...

T L