• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 1:20 PM
MAPISHI KIKWETU: Supu ya broccoli na jibini ya Cheddar

MAPISHI KIKWETU: Supu ya broccoli na jibini ya Cheddar

NA MARGARET MAINA

[email protected]

SUPU ni mlo muhimu wakati wa majira ya baridi.

Supu ya jibini ya Cheddar na broccoli imepata nafasi namba moja kipindi kama hicho kwa sababu watu wengi wanaipendelea.

Nao watoto huipenda kwa sababu ya muundo wake wa krimu na ladha ya jibini.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 15

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • vijiko 4 vya siagi
  • kikombe ½ cha vitunguu maji vilivyokatwa
  • punje 4 za kitunguu saumu zilizokatwa
  • vijiko 4 vya unga wa ngano
  • vikombe 2 vya supu au ya mboga
  • chumvi
  • kijiko ½ pilipili nyeusi
  • kijiko ¼ kungumanga, kwa hiari
  • vikombe 3 vya maua ya broccoli, kata vipande vidogovidogo
  • karoti 3 zilizokunwa na kukatwa vipande vidogovidogo
  • vikombe 2 vya krimu nzito
  • jibini ya Cheddar iliyokunwa

Maelekezo

Yeyusha siagi kwenye ovena au sufuria kubwa juu ya moto wa kati.

Ongeza vitunguu na kaanga kwa dakika muda wa dakika nne au hadi viwe laini na yenye rangi ya kahawia.

Ongeza vitunguu saumu na kaanga kwa dakika moja.

Ongeza unga na koroga kwa muda wa dakika mbili au mpaka unga uanze kugeuka kuwa rangi ya dhahabu.

Mimina supu ya kuku, broccoli, karoti, na viungo.

Chemsha kisha punguza moto kwa kiwango cha wastani na upike kwa robo saa au hadi karoti na majani ya broccoli yaive.

Ongeza jibini ya Cheddar na uweke kwa moto wa chini kwa dakika tatu. Onja na urekebishe viungo ikiwa inahitajika.

Pakua na ufurahie kwa mkate au namna utakayo wewe mwenyewe.

You can share this post!

LISHE: Vyanzo vizuri vya protini ya mimea

MLO MTAMU: Wali, kuku na mkate aina ya naan

T L