• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
LISHE: Vyanzo vizuri vya protini ya mimea

LISHE: Vyanzo vizuri vya protini ya mimea

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WATU zaidi na zaidi wanapenda lishe ya mboga kama njia ya kupunguza matumizi yao bidhaa za wanyama.

Kuhama kutoka kwa bidhaa za wanyama kunakuwa rahisi kwa vyakula vilivyoimarishwa na virutubisho zaidi vinavyopatikana kutoka kwa mimea.

Baadhi ya bidhaa za mimea, kama vile maharagwe ya soya na quinoa, ni protini kamili.

Hii ina maana kwamba zina asidi zote tisa muhimu za amino ambazo wanadamu wanahitaji. Wengine wanakosa baadhi ya asidi hizi za amino, kwa hivyo ni muhimu kula lishe tofauti.

Dengu

Dengu zina protini nyingi, nyuzinyuzi, na virutubisho muhimu, ikiwa ni pamoja na chuma na potasiamu.

Dengu ni chanzo kikubwa cha protini na ndiposa wengi wana mazoe ya kuziongeza kwenye chakula cha mchana au chakula cha jioni. Wanaweza kuziongeza kwenye kitoweo, kari, saladi, au wali ili kutoa sehemu ya ziada ya protini.

Njegere

Njegere ni muhimu sana kama chanzo cha protini.

Karanga

Karanga zina protini nyingi, zimejaa mafuta yenye afya, na zinaweza kuboresha afya ya moyo.

Siagi ya karanga pia ina protini nyingi.

Kwinoa

Kwinoa ni nafaka yenye protini za kiwango cha juu.

Nafaka hii pia ina virutubisho vingine vingi, ikijumuisha magnesiamu, chuma, nyuzinyuzi na manganesi. Pia huwa ni yenye matumizi mengi.

Mbegu za chia

Mbegu za chia zina kiwango cha chini cha kalori na zina utajiri wa nyuzi na asidi ya mafuta ya Omega-3 yenye kuimarisha afya ya moyo. Mbegu za chia ni chanzo kamili cha protini.

Mbegu za chia kwenye maziwa. PICHA | MARGARET MAINA

Jaribu kuongeza mbegu za chia kwenye smoothie, nyunyuzia juu ya mtindi au loweka kwenye maji au maziwa ya mlozi ili kutengeneza pudding.

Maharage na wali

Kwa kando, wali na maharagwe ni vyanzo vya protini visivyo kamili. Kwa kuliwa pamoja, mlo huu wa kawaida unaweza kutoa kiwango kikubwa cha protini.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Teriyaki chicken

MAPISHI KIKWETU: Supu ya broccoli na jibini ya Cheddar

T L