• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Mdalasini na faida zake mwilini

Mdalasini na faida zake mwilini

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MBALI na faida za kiafya ambazo mdalasini hutoa, ni muhimu pia katika urembo.

Mdalasini huongezwa katika vyakula mbalimbali na kukifanya kinukie vizuri pamoja na kuongeza ladha kwa chakula.

Mdalasini huwa na virutubisho na ni chanzo cha madini ya potassium, manganese, calcium, magnesium, zinki na chuma.

Virutubisho hivi husaidia kupunguza shinikizo la damu na viwango vya sukari kwenye damu. Pia hutibu shida za wanawake, magonjwa ya kupumua na shida za kumeng’enya chakula.

Maji ya mdalasini ni muhimu

Maji ya mdalasini pamoja na asali husaidia mtu ambaye anataka kupunguza uzani kwani yanasaidia kuondoa sumu mwilini. Maji ya mdalasini hukufanya ujisikie umeshiba na kuzuia njaa na hamu ya chakula. Hii inasaidia zaidi mtu kupunguza uzani haraka.

Wanawake ambao wana maumivu ya wakati wa hedhi wanaweza kunywa maji ya mdalasini ambayo husaidia kupunguza maumivu hayo. Mdalasini huwa na analgesic na anti-coagulate ambayo husaidia kupunguza maumivu.

Huimarisha kinga

Maji ya mdalasini huwa na antioxidants kama polyphenols na proanthocyanidins ambazo husaidia kuimarisha mfumo wa kinga. Pia, maji ya mdalasini yana anti-fungal, antibacterial na antiviral ambazo hupunguza nafasi za magonjwa kama shida za moyo, magonjwa ya kupumua, na kadhalika.

Huimarisha namna ubongo unavyofanya kazi

Maji yaliyoongezwa mdalasini huboresha kumbukumbu na kuimarisha namna ubongo unavyofanya kazi. Mdalasini huwa na uwezo wa kupunguza kasi ya ukuaji wa magonjwa ya ubongo kama ugonjwa wa Parkinson na Alzheimer’s. Maji ya mdalasini pia husaidia katika kuimarisha umakinifu.

Hupunguza maumivu ya meno

Mara nyingi tunasumbuliwa na maumivu ya meno ambayo hayavumiliki. Mdalasini huwa na chembechembe zenye nguvu ambazo zina uwezo wa kuponya jino linalouma. Kunywa maji ya mdalasini ili kupunguza maumivu ya meno na pia kukabili uvimbe wa ufizi.

Huboresha ngozi

Maji yenye mdalasini husaidia katika kuboresha ngozi. Mdalasini ni chanzo bora cha nyuzi ambazo husaidia kuondoa sumu mwilini. Hii inazuia hali ya sumu kuziba ngozi.

You can share this post!

Siku ya sarakasi kwa Wanjigi, alala ndani licha ya...

Mauaji ya Wakenya kiholela yazidi miili 19 ikipatikana Mto...

T L