• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Mfumo wa Agro Ikolojia kuboresha udongo

Mfumo wa Agro Ikolojia kuboresha udongo

NA SAMMY WAWERU 

AGRO Ikolojia, pia, Kilimo Ikolojia, ni mfumo wa zaraa endelevu unaolenga kuhakikisha matumizi ya pembejeo zenye kemikali yanapunguzwa au yanaepukwa. 

Kimsingi, Sam Nderitu Afisa Mkuu Mtendaji G-GBIACK anauainisha kama mbinu maalum kufanikisha kilimoasilia kwa kutunza afya ya udongo.

Aidha, mbinu hizo zinashirikisha kanuni za Ikolojia, Biolojia, na Sayansi asilia kuzalisha mazao.

Kulingana na mtaalamu huyu mwenye tajiriba ya masuala ya udongo, kurejesha hadhi ya mashamba si tu nchini, bali kote ulimwenguni, ambayo yamelemewa na fatalaiza na dawa zenye kemikali kukuza mimea na kuzalisha chakula, wakulima hawana budi ila kurejelea kilimoasilia. 

Sam Nderitu, mtaalamu wa udongo nchini hutoa mafunzo kuhusu mfumo wa Agro Ikolojia. PICHA|SAMMY WAWEWRU

“Inachukua karibu miaka sita kuharibu udongo, na kuurejeshea hadhi yake si jambo rahisi kama inavyodhaniwa. Muda sawa na huo, unahitajika kuurejesha ulipokuwa,” Nderitu anasema. 

Mboleaasilia, inayojumuisha kinyesi cha mifugo, majani na matawi, na wadudu faafu kusaidia kuiboresha, mdau huyu anasisitiza ndio msingi wa kusuluhisha changamoto za udongo. 

Nderitu, hata hivyo, anaonya mkulima awe makini kuhakikisha mbolea inaiva sambamba. 

“Agro Ikolojia, aghalabu inafanikishwa mkulima akitumia malighafi yaliyo katika mazingira yake badala ya kutoa nje. Wanacholishwa mifugo, awe makini, yasiwe malisho yaliyokuzwa kwa kutumia kemikali. Kinyesi wanachotoa, majani na matawi ya mimea, yatumike kuunda mbolea,” ahimiza.

Mtaalamu huyu anaamini robo ekari ni tosha mkulima kupata chakula cha kutosha, na kujipa mapato. 

  • Tags

You can share this post!

Afisa wa zamani wa magereza asubiri tambiko kabla ya...

Matokeo ya KCPE kutolewa Alhamisi wazazi, wanafunzi...

T L