• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
MUME KIGONGO: Ubora wa mbegu za kiume hufifia kadri umri unavyoongezeka – Utafiti

MUME KIGONGO: Ubora wa mbegu za kiume hufifia kadri umri unavyoongezeka – Utafiti

BAADHI ya wanandoa au wapenzi huamua kupata mtoto au watoto wakiwa na umri mkubwa – labda kupata fursa ya kukamilisha masomo yao na kupata ajira.

Japo huo ni uamuzi wa mtu na mke au mpenzi wake, wanasayansi wanaonya kuwa mbegu za kiume huwa hafifu kadri umri unavyoongezeka.

Kulingana na Dkt Charles Muteshi, mtaalamu wa masuala ya uzazi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, Nairobi, viungo ambavyo huhusika katika utengenezaji wa mbegu huwa dhaifu umri unapoongezeka.

Hiyo ndiyo sababu baadhi ya wazee wameishiwa uwezo wa kutungisha mimba licha ya kufanikiwa kupata watoto wakati wa ujana wao.

Dkt Muteshi anasema kuwa baadhi ya wanaume wa zaidi ya umri wa miaka 50 huzalisha watoto wenye uzani wa chini ya kilo 2.

“Utafiti uliofanywa nchini Amerika ulibaini kuwa idadi kubwa ya watoto wenye umri wa chini ya kilo 2, baba zao walikuwa wazee wa zaidi ya miaka 60. Watoto wanaozaliwa na uzani wa chini huwa katika hatari ya kukumbwa na msururu wa maradhi kwani kingamwili huwa dhaifu,” anasema.

Dkt Muteshi, hata hivyo, anasema kuwa wazee wanaweza kuwa na mbegu za kiume imara iwapo watazingatia lishe ifaayo na kubadili mtindo wa maisha.

“Mwanamume akifanya mazoezi ya mara kwa mara na kupunguza ubugiaji wa pombe, dawa za kulevya na uvutaji wa sigara, anaweza kuwa na mbegu za kiume thabiti hata akiwa mzee,” anashauri Dkt Muteshi.

Anasema kuwa wanaume wanaotamani watoto wakiwa na umri mkubwa wanaweza kwenda hospitalini mbegu zao zihifadhiwe kwa lengo la kudumisha ubora wake.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Tatizo la kigugumizi linakumba zaidi watoto...

Mama akamatwa kwa madai ya kuwekea bintiye dhamana feki

T L