• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Tumia mchele kutengeneza sabuni yenye manufaa tele kwa ngozi

Tumia mchele kutengeneza sabuni yenye manufaa tele kwa ngozi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WENGI wetu tunakula wali lakini inawezekana hatujui kwamba mchele unaotumika kupikia wali unaweza kutengeneza sabuni na inayo faida mbalimbali katika ngozi.

Kuna faida mbalimbali za urembo katika mchele kuanzia kwenye nywele mpaka ngozi.

Sabuni iliyotengenezwa kwa kutumia mchele inasaidia kuifanya ngozi yako iwe laini, kung’arisha ngozi na kadhalika.

Faida za sabuni ya aina hii ni kama vile:

Inasaidia kung’arisha ngozi yako

Inasidia kuipa ngozi yako rangi moja kama utaitumia mara kwa mara. Pia inasaidia kung’arisha sehemu za makovu katika ngozi.

Inasaidia kuipa ngozi unyevu

Kama sabuni hii itakuwa imechanganywa na asali basi inakuwa na uwezo wa kuifanya ngozi yako kuwa laini.

Unatumiaje sabuni ya mchele?

Kama ambavyo unatumia sabuni nyingine unaweza kutumia sabuni hii kwenye uso kwa dakika tatu na kisha kuosha vizuri uso wako.

Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba sabuni hii inaweza kusaidia kutibu chunusi/vipele.

Kama wewe ni mpenzi wa kutumia vipodozi vya asili ambavyo havijachanganywa na kemikali nyingi, basi unaweza kujaribu sabuni aina hii.

Pamoja na hayo, mchele una Vitamini B1, C na E ambazo ni muhimu sana kwenye tiba ya ngozi, kurefusha nywele, na kukinga ngozi isiharibiwe na maradhi.

Mchele kwa msaada wa madini yaliyomo, husaidia kung’arisha ngozi, na kuifanya kuwa nyororo.

Mchele husaidia sana kuondoa weusi chini ya macho au miwani na hata ule weusi kwenye mapaja.

Pia mchele umasaidia kupunguza mwonekano wa michirizi.

Kwenye nywele, maji ya mchele yanasaidia kukuza na kujaza nywele na nywele zinakua zikiwa na afya nzuri.

  • Tags

You can share this post!

Tosti ya stroberi

Rai Wakenya wasiwachague wafisadi Agosti

T L