• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
UDAKU: Kipa De Gea raha tele kuangusha kimalaika

UDAKU: Kipa De Gea raha tele kuangusha kimalaika

Na CHRIS ADUNGO

KIPA David de Gea, 30, sasa ni kidume kamili baada ya mkewe Edurne Garcia kufyatua kimalaika cha kike kwa jina Yanay.

Hata hivyo, shabiki mmoja wa De Gea alikuwa mwepesi wa kutambua jinsi tarehe ya kuzaliwa kwa Yanay (Machi 4, 2021) inavyowiana na mfumo wa kucheza wa timu ya Manchester United; yaani 4-3-2-1.

De Gea na Edurne walitangazia zaidi ya mashabiki wao milioni 12.8 mitandaoni kuhusu ujio wa Yanay, kupitia Instagram mnamo Ijumaa iliyopita.

Wawili hao walipakia picha iliyoonyesha sehemu ya mkono wa Yanay; ambaye kwa mujibu wa jarida la Divinity nchini Uhispania, jina lake linamaanisha ‘mpenzi wangu’.

Jina Yanay pia lina maana ya mwanamke mrembo mwenye ngozi laini inayopendwa na wengi, au tunda bivu linalotomasika kwa wepesi.

Chini ya picha hiyo, De Gea waliandika maneno “Yanay 4.3.21” na kutia emoji zenye mchoro wa moyo.

Kwa wakati fulani, Edurne alilalamikia hatua ya Man-United kutomchezesha mumewe akisema kikosi hicho “kina sura mbaya kama nyuma ya jokofu.”

“Yanay alizaliwa tarehe inayowiana na mfumo unaopendelewa sana na Man-United, wa 4-3-2-1,” akaandika shabiki mmoja aliyejibu ujumbe wa De Gea na mkewe mtandaoni.

Mfumo wa 4-3-2-1 ndio umekuwa tegemeo la kocha Ole Gunnar Solskjaer tangu kiungo Bruno Fernandes atue Old Trafford akitokea klabu ya Sporting Lisbon nchini Ureno, mnamo Januari 2020.

Maandalizi ya kuzaliwa kwa Yanay yalimfanya De Gea kukosa mechi iliyoshuhudia Man-United wakiambulia sare tasa dhidi ya Crystal Palace, ugani Selhurst Park mnamo Jumatano iliyopita.

Mlinda-lango huyo wa zamani wa Atletico Madrid pia alikosa Debi ya Manchester iliyokutanisha Red Devils na majirani wao watani Manchester City, hapo jana uwanjani Etihad.

Inatarajiwa De Gea hatakuwa michumani katika jumla ya mechi tano zijazo huku nafasi yake ikijazwa na kipa Dean Henderson.

De Gea alifichulia mashabiki kuhusu ujauzito wa mkewe Desemba iliyopita, akipakia mtandaoni picha ya chupa ya maziwa ya mtoto, glavu za kipa na kipaza-sauti kilichoashiria taaluma ya muziki ya Edurne.

Chini aliweka michoro ya mtoto mwenye furaha na kuandika: “Mtoto yu njiani.”

Ujumbe huo wa De Gea ambao Edurne alisambaza kwa mamilioni ya wafuasi wake mitandaoni, ulichangamkiwa na mashabiki wengi huku ukisomwa na zaidi ya watu 174,000 chini ya kipindi cha saa moja.

Edurne, 34, ni mwanamuziki, mwigizaji na mwanahabari aliyepata umaarufu zaidi mnamo 2005 kutokana na kipindi chake cha runinga nchini Uhispania, ‘Operacion Triunfo’.

Mwishoni mwa mwaka 2020, Edurne aliwaduwaza sana mashabiki wake kwa kupakia mitandaoni picha zilizoonyesha sehemu kubwa ya uwazi wa makalio, mapaja na maziwa yake kifuani. Kidosho huyo alipigwa picha hizo akiwa ndani ya bwawa la kuogelea huku akizipapasa chuchu zake.

You can share this post!

Uhuru ataweza Raila na Ruto?

DIMBA NYANJANI: Karate ya ‘chini kwa chini’ ya Kenpo...