• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la kuendelea kuvuja damu baada ya kujifungua

UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la kuendelea kuvuja damu baada ya kujifungua

NA PAULINE ONGAJI

TATIZO la mwanamke kuendelea kuvuja damu kutoka ukeni, miezi baada ya kujifungua linafahamika kama Lochia kwa lugha ya kitaalamu, na hutegemea na upesi wa mwili kuondoa uchafu kama kamasi, mabaki ya maji na damu baada ya kujifungua.

Lochia, huwa sawa na kuvuja damu kunakotokea wakati wa hedhi, lakini wakati huu damu hii huwa nyingi sana. Huanza saa kadhaa baada ya kujifungua na huendelea kwa muda wa kati ya wiki mbili na tatu.

Lakini kwa wanawake wengine, shida hii hudumu kwa hata wiki sita.

Dalili za Lochia

Kutokwa na damu nyingi kutoka sehemu ya uke, inayoambatana na migando ya damu

Kisunzi, kuumwa na kichwa na uchovu

Jinsi ya kupambana na hali hii

Pumzika sana huku ukiepuka kusimama na kutembea kwingi

Tumia visodo vizito ili kudhibiti kiwango cha damu kinachotoka

Usitumie visodo vya kuingiza ukeni kwa wiki sita baada ya kujifungua kwani, vyaweza leta bakteria ukeni na hata kusababisha maambukizi.

ITAENDELEA WIKI IJAYO

You can share this post!

PENZI LA KIJANJA: Ukitaka kumjua ‘gold digger’, bana...

Wolves wamtimua kocha Bruno Lage kutokana na msururu wa...

T L